WADAU WA UKATILI SHINYANGA,WAJADILI NAFASI ZA WANAWAKE & WATOTO KWA VYOMBO VYA HABARI.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza kuhusu haki za wanawaka na watoto kwa vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania,Groly Mbia ,akizungumzia kuhusu ushirikiano wa taasii yake na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika miradi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Na Estomine Henry.
Changamoto ya wanawake na watoto kushindwa kujieleza dhidi ya matukio yanayohusiana na ukatili wa kijinsia katika vyombo vya habari yanasababishwa na mila na desturi,mazingira ya mifumo na uwezo binafsi katika kupaza sauti dhidi vitendo hivyo.
Hayo yamelezwa na Mwenyekiti wa Umoja wa asasi za kirai zinazotokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga(SHYEVAWC),Jonathan Kifunda ,leo Mei 18,2023 katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga,yalitoa fursa kwa wadau kuweza kujadili kwa mada ya "Uhuru wa kujieleza kuleta ustawi wa maendeleo mkoani Shinyanga",Ambapo wadau wa ukatili SHYEVAWC walielezea kuhusu uhuru wa kujielezea juu ya haki za wanawake na watoto katika vyombo vya habari.
Jonathan anasema,umoja huo toka uanze umekuwa na matunda kwa kushirikiana na ofisi ya waandishi wa habari mkoani humo kama mwanachama wa umoja huo waliopewa jukumu la kusimamia kitengo cha habari na mawasiliano katika harakati za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
"Vyombo vya habari vinashirikiana nasi vizuri juu ya matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,lakini zipo changamoto ikiwa ni uwezo binafsi wa wanawake kuzungumza na vyombo vya habari au majukwa mengine, mazingira kimfumo na mila na desturi zetu bado zinawafanya wanawake kuona kuwa ni jukumu la wanaume kuongea masuala yote na wao kubaki kuwa kimya"anasema Jonathan
"Vyombo vya habari,vimekuwa vikiibua matukio ya ukatili wa kijinsia katika mkoa wetu,ila bado changamoto ni kuacha kufatiliaji hukumu za kesi hizo ili kurejesha matokeo kwa jamii,Tunaomba vyombo vya vya habari kuweka nguvu hii kwa upande huu tena" anasema Jonathan
Kwa upande Mwingine,Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga,Tedson Ngwale anasema,Shinyanga inafanya vizuri kwa kushirikiana vema na vyombo vya habari juu ya matukio mbalimbali.
"Tutaendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwani ni msaada kwetu kama serikali kwa habari hizo kuwa sehemu ya kumbukumbu katika taarifa za kiofisi ya mkoa wa Shinyanga na vema waandishi wawe na uvumilivu pindi wanapohita habari za masuala ya ukatili kwa ofisi baada ya viongozi wote kuwasiliana"anasema Ngwale.
Naye mratibu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania mkoa wa Shinyanga, Groly Mbia anasema,Klabu ya waandishi shinyanga imefanya vema kuhusu kupaza sauti za wanawake na watoto kupitia miradi ya kutokomeza ukatili,iliyoendeshwa na klabu hiyo kwa ufadhili shirika hilo.
"Tumekuwa kukishirikiana na vyombo vya habari katika kutetea haki za wasichana,wanawake na watoto kwa kuvunja ukimya ili kuwafikia walengwa wa maeneo ya pembezoni"anasema Glory.