Washiriki wa kikao wakiwa katika kikao cha uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama
Meneja wa shirika lisilo la kiserkali la TADEPA Penina Petro(aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama.
Na Elizabeth Charles
WADAU wilayani Kahama mkoani hapa wameshauri jamii,viongozi wa dini pamoja na serikali kuandaa mikakati ya pamoja katika malezi na makuzi ya watoto lengo ikiwa ni kusaidia kukuza viwango vya stadi za maisha na maadili.
Hayo yamebainishwa jana tarehe
25/05/2023 katika uzinduzi wa taarifa ya
mradi wa ALIVE wenye lengo kupima uwezo wa stadi za maisha kwa vijana wenye
umri kati ya miaka 13-17 wilayani Kahama yanayotekelezwa na shirika lisilo la
kiserkali la Milele Zanzibar Foundation kushirikiana na shirika la TADEPA Kahama.
Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa shirika lisilo la kiserikali la TADEPA Penina Petro amesema utafiti umeonesha kuwa watoto wengi bado hawajitambui hali ambayo inawasababisha kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
“Kuna uhitaji mkubwa wa wazazi kuwekeza kwenye malezi na makuzi ya watoto wao lakini pia walimu kule shuleni waendelee kuwafundisha na kuwaelekeza mambo mazuri pia jamii inawajibu wa kushirirkiana na wazazi kulea kwasababu watoto kwa sehemu kubwa wanashinda na katika michezo mbalimbali” amesema Penina.
Kwa upande wake Mwezeshaji katika mradi wa upimaji wa stadi za maisha(ALIVE)Husna Kingu amesema vijana wengi hawana mahiri za stadi za maisha na maadili ambazo ni kujitambua,kutatua matatizo,ushirikiano na maadili ya heshima hivyo kama jamii inatakiwa kuinuka kusaidia watoto.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Kahama Robert Kwela amesema watashirikiana na maafisa elimu msingi waende wakaangalie tatizo liko wapi kwenye ufundishaji.
“Tutaelekezana mpaka na wenzetu kwenye idara ya maendeleo ya jamii na wao washuke kwenye ngazi ya kaya wakusanye taarifa nafikiri tutajua wapi kuna tatizo”alisema kwela.
Mwakilishi wa katibu tawala wilaya ya Kahama Vicent Ndesekio amewataka viongozi kuanzia ngazi ya kata na serikali za mitaa kuandaa utaratibu wa kuzungumza na wazazi na walezi kuhamashisha malezi bora katika familia.
Aidha miongoni mwa mambo yaliyobainishwa kupitia taarifa ya utafiti wa Mashirika hayo ni pamoja na asilimia 68 ya vijana kati ya umri wa miaka 13-17 wilayani Kahama hawana umahiri wa kusoma na stadi za maisha.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Kahama Robert Kwela akizungumza katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17 ) wilayani Kahama
Mwakilishi wa katibu tawala wilaya ya Kahama Vicent Ndesekio akizungumza katika kikao cha uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama
Washiriki wa kikao wakifuatilia uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama
Washiriki wa kikao wakifuatilia uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama