DC KISHAPU AWATAKA WANANCHI KUPAZA SAUTI JUU YA MMOMONYOKO WA MAADILI NA VITENDO VYA UKATILI

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akisalimiana na wananchi walioleta watoto wao clinik kwenye hospitali ya ya wilaya Kishapu

Suzy Luhende,Shinyanga blog

Wananchi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wametakiwa kupaza sauti juu ya Mmomonyoko wa maadili na vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na kukemea mabaya yote yasiendelee kutokea wilayani humo.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude kwenye maadhimisho ya siku ya familia Duniani iliyofanyika leo Mei, 15, 2023 katika Kata ya Kishapu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, viongozi wa Serikali, Chama, sambamba na utoaji wa elimu kuhusu kushuka kwa maadili kwa watoto.

Mkude ambaye alikuwa mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo amewataka wananchi wilayani humo kukemea mabaya yote na kuwafundisha watoto kuhusu maadili mema ili wasijiingize kwenye vitendo visivyo faa katika jamii, na pia amewataka wananchi kupinga masuala ya Mila na Desturi zenye madhara ambazo zinaleta Maadili mabaya kwenye jamii. 

"Kwanza kabisa natoa shukurani za dhati kwa serikali yetu chini ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutambua Jambo hili la familia na kuelekeza tufanye jambo hili kupitia Waziri Mkuu, ambalo tumeanzia, amesema Mkude.

"Tumeenda hospitalini tumekuta mambo mazuri tumekuta wababa wameleta watoto cliniki, ni jinsi gani inaonyesha upendo kwenye familia, hivyo ni wajibu wetu kuwafundisha watoto wetu maadili mema ili wakiwa wanakua wakue kwenye maadili yaliyo mazuri," amesema Mkude.

Diwani wa Kata ya Kishapu Joel Ndettoson amewataka Wananchi kuwapa Elimu watoto kuhusu Maadili mema na kuwakanya kuacha kujiingiza kwenye vitendo viovu ambavyo vinaweza kuwaletea madhara makubwa kwenye Maisha yao.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kishapu Mwajuma Liyanga amewata wazazi kuvunja ukimya kwenye Familia zao licha ya kuwa na majukumu mengi ambayo yanawabana kwa muda mwingi, amewasisitiza wazazi kuwa na muda wa kuzungumza na watoto na kuwaelekeza mambo mazuri ambapo itasaidia sana kwa watoto kuepuka mambo ambayo siyo mazuri kwao.

Hata hivyo Kauli Mbiu katika Maadhimisho hayo ilikuwa ni Imarisha Maadili na Upendo kwa Familia imara.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza katika maadhimisho ya Familia Duniani yaliyofanyika leo Mei, 15, 2023 katika Kata ya Kishapu 
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akisalimia wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwa amembeba mtoto ambaye ni mmoja wa watoto waliopelekwa cliniki
Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Shadrack Kengese akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kishapu Mwajuma Liyanga akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Afisa maendeleo wilaya ya Kishapu Swalala akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese akisalimia wagonjwakatikahospitali ya wilaya ya Kishapu
Wananchi mbalimbali wsliofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu na wengine kuleta watoto wao cliniki 

Mkuu wa wilaya akimsalimia mgonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Kishapu





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464