WANAWAKE WAKIISLAMU WALALANI VITENDO VYA USHOGA NA USAGAJI







Wanawake wa kiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama wakiwa katika kongamano la kulaani vitendo vya usagaji na ushoga katika jamii

Baadhi ya Masheikh wa wilaya ya Kahama wakiwa katika kongamano la wanawake wa kiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama
Mwenyekiti wa wanawake wa kiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama Bi Bahati Ulimwengu.



Sheikh wa wilaya ya Kahama Omary Adam akizungumza katika kongamano la  wanawake wa kiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama
Mwenyekiti wa Bakwata wilaya ya Kahama sheikh Haji Nassoro akizungumza katika kongamano la wanawake wa kiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama
Katibu wa wanawake wa kiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama Bi Tausi Kilonge

Na Elizabeth Charles,Shinyanga

Umoja wawanawake wakiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamefanya kongamano la kulaani vitendo viovu vya usagaji na ushoga vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa na hofu ya Mungu na kuharibu taswira njema ya utamaduni wa mtanzania.

Kongamono limefanyika katika msikiti mkuu wa ijumaa  wa Masjid Nuru  ulipo katika manispaa ya Kahama na kuhudhuriwa na baadhi ya masheikh kutoka katika manispaa hiyo wakiongozwa na Sheikh wa wilaya ya Kahama Omary Adam 

Akizungumza katika na umoja wa wanawake wa kiislamu JUAKITA wilaya ya Kahama  Sheikh wa wilaya ya Kahama Omary Adam amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa watoto ili kuwanusuru na mmomonyoko wa maadili  hususani kujiingiza katika tabia za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ambayo yameendelea kuenea kwa kasi katika jamii.

Kwanza napenda kuwapongeza kwa kuweka adhima ya kuandaa kongamano kwaajili ya kuzungumzia maadili mema kwa sababu miongoni mwa usia aliutoa mtume Muhammad (s.a.w.w) alihusia watu wawe na maadili mema, lakini napenda kuwausieni ninyi wakina mama ndio madrasa ambayo ikiandaliwa vizuri tunakuwa tumeliandaa taifa zuri,kwa hiyo tumieni nafasi yenu kuhakikisha maadili ya hapati mmomonyoko katika nyumba zenu” Alimema sheikh Adamu.

kwa upande wake mwenyekiti wa Bakwata wilaya ya Kahama Sheikh Haji Nassoro ametoa wito unatolewa kwa wanawake na jami kwa ujumla kuwa mabalozi wa kutoa taarifa zauwepo wa viashiria vyovyote vya mazingira yasiyo rafiki na tatanishi kwa vyombo husika ili kufichua vitendo hivyo na wasika kuchukuliwa hatua.

Mkiona nyumba huko mtaani haieleweki inaingiza vijana wakiume na wakike toeni taarifa kwa vyombo vya dola janga hili mama na dada zangu halibagui, halijui huyu ni muislamu au huyu ni mkristo hivyo wakina mama tunawategemea ninyi maana ndio mhimili kuu na mna wajua watoto kuliko sisi akina baba”ameeleza Sheikh Nassoro.

Katika hatua nyingine viongozi wa umoja wawanawke wa kiislamu juakita wilaya ya kahama wakiongozwa na sheikh Amiri Fadhiri wamesema mapambano dhidi ya mmomonyoko wa maadili ni endelevu na kupitia umoja wao wamekuwa wakiwafikia wanawake wengi kutoka katika wilaya jirani kwa lengo lakupeana elimu ya kidini lakini pia namna ya kuendelea kuimarisha maadili mema katika familia na jamii kwaujumla.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464