ZAIDI YA WABUNIFU 700 WAOMBA MTAJI BENKI YA CRDB KUPITIA IMBEJU



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo akizungumzaa na waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo ya program ya Imbeju inayolenga kutoa mitaji wezeshi kwa wajasiriamali wenye ubunifu wa kiteknolojia zikiwa zimepita wiki tatu tangu kufungwa kwa maombi kwa upande wa biashara bunifu za vijana, katika mkutano uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam. Jumla ya maombi 706 yalikuwa yamepokelewa na kuchakatwa na 196 yakathibitika kukidhi vigezo vya kuingia hatua ya pili itakayowataka waombaji kuwasilisha na kuyatetea mawazo yao. Program hiyo inayosimamiwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation inatekelezwa kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Pamoja na Tume ya Tehama (ICTC).
Mhandisi Jason Ndaguzi wa Tume ya TEHAMA, akizungumzaa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya program ya Imbeju inayolenga kutoa mitaji wezeshi kwa wajasiriamali wenye ubunifu wa kiteknolojia zikiwa zimepita wiki tatu tangu kufungwa kwa maombi kwa upande wa biashara bunifu za vijana, uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.


Dar es Salaam. 02 Mei 2023: Ukiwa umepita mwezi mmoja wa kuwatambua wabunifu wanaotaka kuendeleza miradi yao, Benki ya CRDB imepokea zaidi ya maombi 700 ya wajasiriamali wanaotaka mitaji.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo alipozungumza na waandishi wa habari leo ktika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Benki hiyo.

“Ninapenda kuwajulisha kuwa hadi Aprili 12 dirisha la maombi lilipofungwa, jumla ya maombi 709 yalipokelewa yakiwamo 369 yaliyopitia COSTECH na 340 kupitia ICTC. Kipekee kabisa nimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kutupa heshima ya kutuzindulia na kutufungulia dirisha la maombi kwa vijana na wanawake alioufanya Machi 12 mwaka huu,” amesema Kiondo.

Tangu kuzinduliwa kwa Program ya Imbeju yenye kaulimbiu ya “Mtaji Wezeshi kwa Vijana na Wanawake” inayotekelezwa kupitia taasisi ya CRDB Bank Foundation, dirisha la kupokea maombi ya wabunifu wanaomiliki biashara changa lilifunguliwa ili kuwawezesha kwa mtaji, ujuzi wa kitaaluma na masoko vijana na wanawake wanaozimiliki.

Kupokea maombi, Kiondo amesema ilikuwa ni hatua ya kwanza inayohusisha kutoa mafunzo, ushauri, na mitaji wezeshi kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Pamoja na Tume ya TEHAMA (ICTC).

“Katika kipindi cha mwezi huo mmoja, vijana walipewa fursa ya kuwasilisha maombi ya ushiriki. Maombi yalipokelewa kutoka mikoa yote. Asilimia 70.6 ya maombi yaliyopokelewa yalitoka kwa vijana wanaume na asilimia 29 yalikuwa ya wanawake. COSTECH imeyapitisha maombi 116 na ICTC 80,” amesema Kiondo.


Kaimu mkurugenzi huyo amefafanua kuwa sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa Taifa imeongoza kwa kuwa na asilimia 31 ya maombi yote ikifuatiwa na sekta ya uzalishaji yaani “manufacturing” ikiwa na asilimia 14 huku biashara ya mtandaoni yaani “e-commerce” yakichukua asilimia 18 ya maombi yakifutatiwa kwa karibu na sekta ya teknolojia ya masuala ya fedha yaani “Fintech” kwa asilimia 13.

“Kwa ambao hawajafanikiwa, niwasihi wasikate tamaa kwani programu ya Imbeju ni endelevu, hivyo wajipange kwa dirisha lijalo. Kutochaguliwa kwao kwenda hatua inayofuata sio kwamba tunawaacha hivihivi, Benki inawapa fursa ya kufungua akaunti ya Imbeju yenye faida lukuki zitakazowasiaidia kusimamia vizuri biashara zao ikiwamo mifumo ya malipo na bima ya biashara, na Maisha,” amefafanua Kiondo.
Mkurugenzi wa Ubunifu na Teknolojia kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Gerald Kafuku amesema ukosefu wa mtaji ndicho kikwazo cha wabunifu wengikuingiza bidhaa zao sokoni hivyo akaishukuru Benki ya CRDB kwa kufungua milango ili kuwawezesha.

“Kwa kawaida, COSTECH huwa inatoa ruzuku ya kuendeleza mawazo ya wabunifu. Kwa hatua hii inayotekelezwa na Imbeju, ni kwamba wabunifu wapo tayari kuingia sokoni na wanachokihitaji ni mtaji wa uzalishaji. Kwa muda mrefu, wabunifu hawa walikuwa hawakaopesheki kutokana na kutokuwa na dhamana, naishukuru Benki ya CRDB kwa kuwaondolea kikwazo hicho,” amesema Dkt. Kafuku.

Kwa upande wake, Mhandisi Jason Ndaguzi aliyemwakilisha mkurugenzi mtendaji wa Tume ya TEHAMA amesema wamepata uzoefu mkubwa na wa aina yake wakati ya kuyachakata maombiya wabunifu waliojitokeza hivyo wataboresha mikakatiyaokukuza Zaidi ubunifu nchini.

“Ili kutanua wigo, tumeanza kusajili miradiya wanafunzi wa mwaka w amwisho wa vyuo vikuu. Tunataka kuweka kanzidata ya maeneo wanayoyatafiti ili ikitokea fursa ya kupata mtaji kama ilivyo kwenye program hii ya Imbeju iwe rahisikuwapata wabunifu,” amesema Mhandisi Ndaguzi.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464