WAJUMBE WDC MJINI WATEMBELEA MIRADI INAYONG'ARISHA MJI WA SHINYANGA

Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa maegesho ya bajaji na pikipiki na Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC

                     Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Diwani wa kata hiyo Mhe. Gulam Hafeez Mukadam imetembelea miradi inayotekelezwa katika kata ya Mjini ikiwemo ujenzi wa Bustani za kupumzikia, Maegesho ya Pikipiki na Bajaji , Stendi ya Hiace, Soko Kuu, Soko la Wajasiamali, mitaro na madarasa na vyoo katika shule ya Awali na Msingi Mwenge.

Ziara hiyo imefanyika leo Jumatano Juni 7,2023 ambapo Wajumbe wa kamati ya WDC Kata ya Mjini wameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kata hiyo ambayo ndiyo inabeba muonekano wa Mji wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Diwani wa kata ya Mjini Mhe. Gulam Hafeez Mukadam amesema katika maeneo yote ya miradi waliyotembelea wananchi wameeleza kuridhika na kufurahia miradi ya maendeleo inayotekelezwa ambayo kwa kiasi kikubwa imefanya Manispaa ya Shinyanga kubadilika na kuwa na mandhari yanayovutia na kupendeza.
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa ujenzi wa Soko Kuu Mjini. Shinyanga

“Kutokana na kasi nzuri ya utekelezaji wa miradi katika kata yetu kwa kweli mji wetu unapendeza sana. Ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu kuona Mji wa Shinyanga unabadilika. Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satur ambaye sasa amehamishiwa jijini Dar es salaam amefanya kazi kubwa sana kuleta mabadiliko katika Manispaa yetu”,amesema Mukadam.

“Wana Shinyanga tutaendelea kumkumbuka Satura kwa mabadiliko makubwa aliyoyafanya katika Manispaa ya Shinyanga kwa muda mfupi. Mji wa Shinyanga umependeza kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mkurugenzi Jomaary Satura katika usimamizi wa fedha za serikali na mapato ya ndani. Tunaomba Mkurugenzi anayekuja aendeleze mazuri haya”,ameongeza Mukadam.

Katika hatua nyingine, Mukadam amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo katika shule.

Pia Diwani huyo wa kata ya Mjini ameahidi kufuatilia na kutekeleza miradi iliyokuwa imekwama huku akiahidi kuboresha michezo katika shule zilizopo katika kata hiyo na kuangalia uwezekano wa kutafuta wafadhili ili kujenga ghorofa katika shule ya awali na msingi Mwenge ambayo pia alisoma mwaka 1969 kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa madarasa.

Aidha amekemea vitendo vya ushoga na usagaji na kutaka kila mmoja kupinga vitendo hivyo ili kuwa taifa lenye amani na kizazi salama.
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC wakati Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini ikitembelea miradi mbalimbali leo Jumatano Juni 7,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mtendaji wa kata ya Mjini Mathias Salu akisoma taarifa ya mradi wa bustani ya kupumzikia
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC
Mwendesha bodaboda, Peter Charles akieleza namna walivyofurahia kujengewa eneo la maegesho ya pikipiki na bajaji wakati Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa maegesho ya bajaji na pikipiki katika eneo la Mataa NBC
Mwenyekiti wa Waendesha Bajaji eneo la Phantom, Jailan Ramadhani akieleza namna walivyofurahia kujengewa eneo la maegesho ya pikipiki na bajaji wakati Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa maegesho ya bajaji na pikipiki
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC
Muonekano wa sehemu ya Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC
Muonekano wa sehemu ya Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Mataa NBC
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa Bustani ya kupumzikia iliyopo eneo la Kalogo

Mwalimu Mkuu wa shule ya awali na msingi Mika Kakema akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika shule ya awali na Msingi Mwenge wakati Kamati ya Maendeleo kata hiyo ikitembelea ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo katika shule hiyo.

Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akitembelea ujenzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo katika shule ya awali na msingi Mwenge.
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akitembelea shule ya awali na msingi Mwenge.
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza na mmoja wa wakusanya ushuru katika Stendi ya Hiace, Bajaji na Pikipiki Soko Kuu Mjini Shinyanga.
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa ujenzi wa Soko Kuu Mjini. Shinyanga
Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea mradi wa ujenzi wa Soko Kuu Mjini Shinyanga
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akisalimiana na wananchi wakati Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mjini Manispaa ya Shinyanga ikitembelea Stendi ya Hiace Soko Kuu na mradi wa ujenzi wa Soko Kuu Mjini Shinyanga
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akiwa katika Stendi ya Hiace Soko Kuu na mradi wa ujenzi wa Soko Kuu Mjini Shinyanga
Moja ya mitaro iliyojengwa katika kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga 
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam na wajumbe wa kamati ya WDC wakizungumza na wajasiriamali katika Soko la Wajasiriamali lililopo jirani na Ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464