Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imeadhimisha siku ya Mtoto Afrika kwa kuendesha Tamasha la Junior Jumbo kwa ajili ya utoaji elimu wa masuala ya fedha kwa watoto, wazazi na walezi sambamba na elimu ya bidhaa na huduma za benki ya CRDB ambapo watoto wamejumuika kufurahi na kujifunza masuala ya elimu ya fedha.
Tamasha la Junior Jumbo lililoandaliwa na Benki ya CRDB limefanyika leo Jumamosi Juni 17,2023 katika Viwanja yya Shule ya KOM Mjini Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Akizungumza wakati wa Tamasha hilo, Mndeme ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa tamasha hilo akisema kuwa ni kweli ni Benki inayosikiliza na kujali wateja wake wa kira rika na kwamba baada ya tamasha hilokutakuwa na mabadiliko makubwa kwa kujenga uelewa ambao utawawezesha kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya Benki ya CRDB.
“ Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu na kupelekea kuja na wazo hili la kutoa elimu ya masuala ya fedha hasa kwa watoto kwani sote tunatambua kuwa hawa ndio Taifa la kesho na wahenga wanasema “Samaki Mkunje, Angali mbichi. Benki yetu ya Kizalendo ya CRDB imekua ikifanya jitihada kubwa katika kuimarisha ustawi wa jamii yetu”,amesema Mhe. Mndeme
Amesema ni ukweli ulio wazi kuwa elimu ya fedha ina mchango mkubwa sana katika ukuaji na maendeleo ya uchumi, kujenga uchumi jumuishi, na kupunguza viwango vya umasikini ndiyo maana Serikali kote duniani zimekuwa zikitilia mkazo suala la utoaji wa elimu ya fedha (financial literacy) kwa wananchi.
“Hapa nchini, Serikali, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kisera ili kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya fedha na kukuza ujumuishi wa kifedha kwa wananchi. Sera na Mifumo hii yote imeweka mkazo mkubwa katika masuala ya elimu ya fedha ikitambua umuhmu wake katika kujenga ustawi, wa mtu mmoja mmoja na hata wa jamii kwa ujumla”,amesema Mndeme.
“Tunambua kuwa ili kufikia malengo tuliyojiwekea kama taifa katika Dira ya Maendeleo, inatuhitaji kuwajengea watu wetu uwezo hasa wa elimu ya fedha ili waweze kutambua fursa zilizopo na kushiriki kikamilifu, lakini vilevile tunaamini kuwa ili kufanikiwa katika hili ni lazima tuanzie chini kwa kuanza kuwapa watoto wetu elimu juu ya fedha na kuwajengea tabia ya kujiwekea akiba”,ameongeza Mndeme.
Amesema ili kujenga Taifa lililo imara kiuchumi, ni vyema kuanza kwa kuwekeza katika kuwapatia watoto wetu elimu ya fedha, kwani elimu ya fedha ndiyo inaleta msukumo mkubwa katika kufikia malengo ya kiuchumi.
“Elimu ya fedha huathiri tabia ya kifedha kwasababu mara nyingi inakuwa ni msukumo kutoka ndani, ambao humchochea mtu kufanya maamuzi kulingana na yeye anavyofahamu. Hii inamaanisha watu wasio na msingi imara na ambao wamekuwa na uelewa mdogo juu ya masuala ya fedha wamekuwa wakipata athari hasi kwa maana ya kufanya maamuzi ya kifedha yasiyo na manufaa au muda mwengine kutofanya maamuzi kabisa kutokana na kukosa uelewa”,ameeleza Mkuu huyo wa Mkoa.
Amesema Elimu ya fedha inawapa watoto stadi muhimu za maisha ambazo zitawasaidia katika maisha yao yote kwa kuwajengea uwajibikaji wa kifedha, kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba, na kuwaweka katika njia sahihi ya maendeleo binafsi kufikia uhuru wa Kifedha (financial freedom).
“Lakini nimefurahishwa zaidi kuona malengo ya akaunti ya Junior Jumbo yameunganishwa na kufanikisha ndoto za wototo wetu katika elimu. Upo usemi unaosema urithi bora kwa mtoto ni elimu, leo naomba niongezee hapa kwa kusema kuwa “Urithi bora una jumlisha kuweka misingi bora ambayo itasaidia mtoto kupata elimu na mahitaji yake ya msingi kwa uhakika”,amesema
“Hivyo niwapongeze sana Benki ya CRDB kwa kulitambua hili na kuwawezesha wazazi kufanikisha ndoto za watoto wao katika elimu Akaunti hii ya Junior Jumbo (JJ) kwa kuwawezesha kuweka Akiba kidogo kidogo ili kufikia lengo. Niwapongeze pia kwa hamasa ambayo mmekuwa mkiitoa kwa wazazi kupitia kampeni mbalimbali ikiwamo hii ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” ambayo pia inatoa fursa ya wazazi kujishindia ada kwa ajili ya waoto. Huu ni ubunifu mkubwa ambao unapaswa kupongezwa”,ameongeza.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiweka mazingira wezeshi katika sekta ya kuhakikisha watoto wote wanapata elimu kupitia sera ya ‘elimu bure’, lakini mahitaji ya kuhakikisha mtoto anapata elimu bora yanajumuisha vitu vingi ambavyo pia ina mhitaji mzazi kujipanga kifedha. Hivyo basi hii ni fursa nzuri sana ambayo inapaswa kila mzazi au mlezi kuitumia.
Mkuu huyo wa mkoa pia amewasihi Wazazi na Walezi kuweka mikakati madhubuti ya kuweka akiba kwa ajili ya watoto kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutimiza majukumu yao kama wazazi kwa maana ya kumudu mahitaji ya watoto pamoja na kuwawezesha kufikia malengo waliyojiwekea ili kujenga Taifa bora zaidi siku za usoni.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya Magharib Benki ya CRDB, Jumanne Wagana Benki ya CRDB inachukulia kwa umuhimu mkubwa suala la kuwatengenezea mazingira yaliyo bora watoto wetu, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwawezesha kutimiza malengo yao pamoja na kuandaa taifa lililo imara hapo baadae.
“Tukiwa sehemu ya familia kubwa ya Watanzania, Benki yetu inaamini katika uwajibikaji wa kifedha “responsible finance”, lakini vilevile tunaamini kuwa ili kufanikiwa katika hili ni lazima kuanza kuwapa watoto wetu elimu juu ya fedha na kuwajengea tabia ya kujiwekea akiba. Kuwafundisha watoto juu ya tabia njema za utunzaji wa fedha kunawapa fursa ya kufanikiwa wakiwa wakubwa",amesema Wagana.
“Umekuwa utamaduni wetu watanzania kuwafundisha watoto wetu juu ya mambo mbalimbali katika maisha, lakini watoto walio wengi wanakosa elimu juu ya fedha “Financial Education” na kujiwekea akiba, elimu ambayo ni muhimu sana kwa watoto na vijana wetu. Elimu ya fedha huwapa watoto uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali za kifedha na kuwapatia uwezo wa kufanya maamuzi sahihi”,amesema Wagana.
“Kwa kutambua umuhimu wa elimu ya fedha kwa watoto na umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya watoto hususan katika kuwasaidia kufikia ndoto zao kupitia elimu, Benki yetu ya CRDB hivi karibuni imezindua kampeni maalum ya “Timiza Ndoto yake na JJ” kupitia akaunti ya “Junior Jumbo”.
Kampeni hii inalenga katika kutoa elimu ya fedha kwa watoto, pamoja na kuwahamasisha wazazi/ walezi juu ya umuhimu wa kuwawekea watoto wao akiba”ameeleza.
Amesema Akaunti ya Junior Jumbo “JJ” ni akaunti ambayo imebuniwa mahsusi ili kuwasaidia wazazi/walezi katika kutimiza ndoto za watoto wao hususani katika elimu. Hii ni akaunti ya malengo ambayo inamuwezesha mzazi kumuwekea akiba mtoto kidogo kidogo ili kutimiza malengo aliyojiwekea kwa mtoto.
“Akaunti ya hii ya Junior Jumbo ina faida mbalimbali mfano Mteja ana uhuru wa kuchagua aina ya sarafu anayotaka kuendeshea akaunti (TZS, USD, EURO, GBP). Akaunti hii inafunguliwa kwa kiwango nafuu sana ambapo kiwango cha chini ni shilingi 20,000 / 20 USD, EURO, GBP na Akaunti ya Junior Jumbo haina gharama yoyote ya uendeshaji”,amesema Wagana.
Faida zingine ni kwamba Mteja hunufaika na riba nzuri inayolipwa kila mwaka, Mzazi au mlezi anaweza kuweka agizo la kuhamisha fedha (standing order) kwenda akaunti ya Junior Jumbo bure, Huwajengea watoto tabia njema ya kupenda kujiwekea akiba na hivyo kupata ufahamu juu ya elimu ya fedha na hurahisisha zoezi la kuwekeza fedha kwa ajili ya mahitaji ya watoto.
Kampeni ya “Timiza Ndoto yake na JJ” ni sehemu ya jitihada kubwa zinazofanywa na Benki yetu ya CRDB katika kuhamaisha na kuchochea wazazi/ walezi wengi zaidi kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya watoto huku akiongeza kuwa tangu kuanzishwa kwake akaunti ya Junior Jumbo imepokelewa vizuri sokoni kwani hadi kufikia mwezi Mei mwaka 2023 akaunti zaidi ya 180,000 zenye amana ya zaidi ya Tsh billioni 133 zimefunguliwa .
“Kupitia kampeni hii ya mwezi mmoja, Benki inatoa zawadi za ada za shule “School Fees” kwa wazazi ambao wamewafungulia watoto wao akaunti ya Junior Jumbo na kuweka akiba mara kwa mara katika kipindi cha kampeni.
Zawadi zitatolewa kwa jumla ya washindi 21, washindi watatu kutoka kila kanda katika kanda zetu saba. Mshindi wa kwanza katika kila kanda atajishindia Shilingi Milioni 1, mshindi wa pili Shilingi laki 7, na mshindi wa tatu Shilingi laki 5, hivyo kufanya jumla ya zawadi za Shilingi milioni 15.4. Kushiriki katika kampeni hii”,ameongeza Wagana.
“Katika kipindi hiki cha kampeni Benki pia inaendelea na utaratibu wake wa kufanya matamasha ya “Junior Jumbo” katika kanda zetu kama ambavyo tumekutana leo hii hapa tukiwa na lengo la kutoa elimu ya fedha kwa watoto na wazazi/walezi. Tunafurahi sana kuona mwitikio umekuwa mkubwa na sisi tumejipanga vilivyo kutoa elimu na kuwaunganisha na fursa zinazotolewa na Benki yetu ya CRDB”,amesema.
Wagana amewahamasisha wazazi na walezi ambao bado hawajawafungulia watoto wao akaunti ya Junior Jumbo, waitumie fursa hiyo vizuri, ili kuanza kuwajengea watoto utamaduni wa kujiwekea akiba, na uwelewa juu ya masuala ya kifedha na kwa ambao wana akaunti amewahimiza kuweka akiba kwa watoto wao, na kuwafundisha pia wao wenyewe kuweka akiba.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa maadhimisho ya Mtoto wa Afrika kwenye Tamasha la Junior Jumbo lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto.
Kaimu meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiendelea kusajili watoto kwenye Akaunti za watoto maarufu Junior Jumbo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto.
Mkuu wa mkoa wa hinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto.
Mkurugenzi wa shule za KOM Jackton Koy akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi wa wazazi Alfred Kailembo akizungumza kwaniaba ya wazazi.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bakari Kasinyo akizungumza.
Mkurugenzi wa shule ya Hilbat Dkt Clement akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi shule za binafsi.
Watoto wakitoa burudani
Mchekeshaji maarufu Brother K kutoka Futuhi akitumbuiza
Mkuu wa mkoa wa hinyanga Christina Mndeme akimkabidhi zawadi mchekeshaji Brother K (kulia).
Mkuu wa mkoa wa hinyanga Christina Mndeme kushoto akimkabidhi zawadi mchekeshaji Brother K
Mshereheshaji MC Mzungu akisherehesha.
Watoto wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya watoto waliohudhuria maadhimisho hayo.
Baadhi ya watoto waliohudhuria maadhimisho hayo.
Baadhi ya wazazi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mkuu wa mkoa wa hinyanga Christina Mndeme akizungumza na watoto.
Mchekeshaji Brother K Akitumbuiza kwenye maadhimisho.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Picha ya pamoja shule ya msingi Sheer Bliss na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Picha ya pamoja shule ya msingi Samuu na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Picha ya pamoja shule ya KOM na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Picha ya pamoja shule ya msingi Ibaadhi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Picha ya pamoja wafanyakazi wa CRDB na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Picha ya pamoja baadhi ya wazazi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme