SHINYANGA YAENDESHA KIKAO CHA KUWAJENGEA UWEZO WADAU NA MAAFISA KATIKA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YA RAIS SAMIA YA MSAADA WA KISHERIA


Msajili Msaidizi wa watoa huduma ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao hicho na kuelezea malengo mahususi ya kampeni ya Rais Samia ya msaada wa kisheria.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SERIKALI mkoani Shinyanga imeendesha kikao cha kuwajengea uwezo Wadau na Maafisa katika utekelezaji wa kampeni ya Rais Samia ya msaada wa kisheria, ambayo uzinduzi wake Rasmi mkoani humo utafanyika Juni 11 mwaka huu.

Kikao hicho kimefanyika leo Juni 7, 2023 na kukutanisha, Watendaji wa Kata kutoka Halmashauri Sita za Mkoa wa Shinyanga, Maofisa Maendeleo, Wakuu wa idara, Wasaidizi wa Kisheria, Maafisa sheria, na Mawakili kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika Kanda ya Shinyanga (TLS).

Msajili Msaidizi wa watoa huduma ya msaada wa Kisheria mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, amesema kampeni hiyo ya Rais Samia ya msaada wa kisheria, imelenga kusaidia Wananchi kupata huduma za kisheria bure ambao hawawezi kumudu gharama za kulipa Mawakili na kupata haki zao.

Amesema uanzishwaji wa kampeni hiyo ya huduma ya msaada wa kisheria, itaimarisha mfumo wa kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kupata haki zao, bila ya kusubiri matatizo yao kuyawasilisha katika ziara za viongozi wa kitaifa sababu yatakuwa tayari yameshapatiwa ufumbuzi.

"Matokeo ya kampeni hii ni kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu upatikanaji wa huduma ya msaada wa kisheria na kupata haki zao kwa wakati, kupungua kwa idadi ya migogoro itikanayo na uvunjifu wa haki,"amesema Ngwale.

Aidha, amesema kampeni hiyo pia itakwenda kuondoa madhila ambayo wamekuwa yakiyapata wanawake na watoto hasa katika kutendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambapo wahusika watakuwa wakichukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kampeni hiyo ya huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi itatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu, kuanzia mwaka huu 2023 hadi 2026 kwa Tanzania Bara na Zanzibar, ikiwa na Kauli Mbiu isemayo’ Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya huduma ya msaada wa kisheria mkoani Shinyanga John Shija, amewataka wasaidizi wa msaada wa kisheria wasiwe wanaharakati, bali wafanye kazi zao kwa weledi na kusaidia watu kupata haki zao bila ya kutanguliza pesa mbele.

Nao baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho, wamesema kampeni hiyo ya huduma ya msaada wa kisheria itakuwa mkombozi kwa wanyonge, sababu baadhi ya wananchi wamekuwa wakishindwa kupata haki zao kutokana na ukosefu wa Rasilimali fedha kwa ajili ya kuweka Mawakili katika kesi zao.
Msajili Msaidizi wa watoa huduma ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao hicho na kuelezea malengo mahususi ya kampeni ya Rais Samia ya msaada wa kisheria.
Msajili Msaidizi wa watoa huduma ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao hicho na kuelezea malengo mahususi ya kampeni ya Rais Samia ya msaada wa kisheria.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga John Shija akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujengewa uwezo kwa ajili ya kampeni ya Rais Samia ya msaada wa kisheria, ambayo Mkoani Shinyanga itazinduliwa Rasmi Juni 11 mwaka huu.
Mawakili kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika Kanda ya Shinyanga (TLS)wakiwa kwenye kikao hicho.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
kikao kikiendelea.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
kikao kikiendelea.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujengewa uwezo kwa ajili ya kampeni ya Rais Samia ya msaada wa kisheria, ambayo Mkoani Shinyanga itazinduliwa Rasmi Juni 11 mwaka huu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464