KAMATI YA BUNGE YAFUNGUKA MIKATABA YA BANDARI


Kamati yashauri mikataba itakayosainiwa itaje muda wa utekelezaji


Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeshauri mikataba ya utekelezaji itakayosainiwa itaje muda maalumu wa utekelezaji wa miradi ambao utazingatia maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.

Dar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeshauri mikataba ya utekelezaji itakayosainiwa itaje muda maalumu wa utekelezaji wa miradi ambao utazingatia maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.


Ushauri huo umetolewa leo Jumamosi Juni 10, 2023 bungeni Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo, Selemani kakoso wakati akitoa maoni ya kamati kuhusu azimio la Bunge kuridhia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania.


Soma hapa zaidi Chanzo Mwananchi

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464