WAZEE,VIONGOZI WA DINI NA MACHIFU SHINYANGA WAMETOA TAMKO KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA MKATABA UWEKEZAJI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Chifu Charles Njange Kidola akisoma Tamko

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZEE, viongozi wa Dini na Machifu mkoani Shinyanga wametoa Tamko la kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan Juu Mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam baini ya Tanzania na Dubai.

Wametoa Tamko hilo leo Juni 16, 2023 kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ambacho kilikuwa na lengo la kupewa elimu juu ya faida za uwekezaji wa Bandari hiyo, pamoja na fedha ambazo zimetolewa na Rais Samia za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo mkoani humo.

Chifu Charles Njange Kidola, akisoma Tamko hilo amesema baada ya Mkuu wa Mkoa kuwapatia elimu juu ya faida za Uwekezaji wa Bandari kwa pamoja wameamua kumuunga Mkono Rais Samia, na kulaani watu ambao wamekuwa wakipotosha Wananchi kupitia mitandao ya kijamii juu ya Mikataba ya Bandari.

“Sisi Wazee,Viongozi wa dini na Machifu wa Mkoa wa Shinyanga tunabariki na kuunga mkono makubaliano ya Mkataba baini ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendeshaji na uboreshaji kazi wa Bandari ya Dar es salaam,”amesema Chifu Kidola.

“Tuna ahidi kuwa Mabalozi wema kutoa elimu hii ya uwekezaji wa Bandari katika maeneo yetu, na tunampongeza Rais Samia kwa kuendelea kutupambania na kutuletea maendeleo Watanzania na Mkoa wetu kwa ujumla,”ameongeza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewaomba Wazee, Viongozi wa Dini na Machifu mkoani humo na Watanzania kwa ujumla, kumuunga mkono Rais Samia Juu ya uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam, na kupuuza maneno ya upotoshaji kwa baadhi ya watu ambao hawana nia njema na maendeleo ya Taifa.

Aidha, akielezea fedha ambazo zimetolewa na Rais Samia Juu ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo mkoani humo, amesema hadi kufikia Juni 16 mwaka huu kimeshatolewa kiasi cha fedha Sh.bilioni 612.3

Amesema katika Sekta ya Elimu Rais Samia ametoa fedha Sh.bilioni 47, Sekta ya Afya Sh. bilioni 26, Miundombinu ya Barabara kwa upande wa Tarura Sh.bilioni 8, Tanroads Sh.bilioni 16.2, Sekta ya Nishati Sh.345, Maji Sh.bilioni 100, TASAF Sh. bilioni 6, Utawala Sh.bilioni 15, na Uwanja wa ndege Sh. bilioni 49.

Katika hatua nyingine amesema Serikali chini ya Rais Samia imendelea kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na kwamba kwa upande Kahama tayari kuna eneo la Hekali 2,000 ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Bandari Kavu, pamoja na eneo ambalo lilikuwa la Mgodi wa Buzwagi Hekta 1,333 limegeuzwa kuwa kitovu uchumi na litaitwa ‘Samia Special Economic Zone.’ Lengo likiwa na kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiongoza kikao chake na Wazee, Viongozi wa Dini na Machifu mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye kikao hicho.
Chifu Charles Njange Kidola akisoma Tamko.
Chifu Charles Njange Kidola akisoma Tamko.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini, Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichangia kwenye kikao hicho.
Mchungaji wa Kanisa la FPCT Galilaya kutoka wilayani Kahama Kagoma Kasagamba akichangia kwenye kikao hicho.

Chifu Nshoma Haiwa akichangia mada kwenye kikao hicho.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Chifu Charles Gambaseni akichangia mada kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wilayani Kishapu Suzana Masebu akichangia mada kwenye kikao hicho.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Katibu wa Chama cha Wazee wanaume Nsolo Stephen akichangia mada kwenye kikao hicho.
Wazee wakiendelea kuchangia mada kwenye kikao hicho.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.

Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini,Wazee na Machifu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464