WAZAWA WAPEWA FURSA NA MGODI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KWA WANANCHI KUPITIA FEDHA ZA CSR

Wazawa wapewa fursa na Mgodi kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

MGODI wa Barrick Bulyanhulu ambao upo Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, umeendelea kuwajengea uwezo wananchi wa vijiji 14 ambao wanauzuka Mgodi huo kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Mgodi pamoja na kupata kazi ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Mrakibu kutoka Idara ya Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu William Chungu, amebainisha hayo jana wakati Waandishi wa habari walipotembelea kuona miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kwa wananchi kupitia Mgodi huo.
Mrakibu kutoka Idara ya Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu William Chungu.

Amesema Mgodi huo ulianzisha Program ya kutoa mafunzo kwa wananchi wa vijiji 14 ambavyo vinauzunguka Mgodi huo kila Jumamosi, ili kutambua fursa zilizopo ndani ya Mgodi na kuzichangamkia ili wajikwamue kiuchumi.
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Bushing'we ambayo inajengwa na Wazawa lakini siyo kwa fedha za CSR.

“Miradi mingi ya maendeleo ambayo tunaitekeleza kwa wananchi kupitia fedha za ‘CSR’ inajengwa na Wazawa na kuzingatia Sera ya (Local Content).

" Zahanati hii ya Bushing'we kama mnavyoona ina jengwa na Wazawa, lakini siyo kwa fedha za CSR ni Mgodi tu umeamua kuikamilisha ili wananchi wapate huduma za afya karibu, lakini tumewapa kazi hii Wazawa" amesema Chungu.
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Bushing'we.

Naye Thomas Mshilu ambaye ni msimamizi wa miradi kutoka Kampuni ya Mjasilia ya Kizawa, ambao wanajenga Zahanati ya Kijiji cha Bushing’we Halmashauri ya Msalala, ameupongeza Mgodi huo kwa kutoa fursa kwa Wazawa, na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi na kuwainua kiuchumi.
Naye Thomas Mshilu ambaye ni msimamizi wa miradi kutoka Kampuni ya Mjasilia ya Kizawa.

Aidha, Msimamizi wa vijiji 14 ambavyo vinauzunguka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Joseph Rubega, amesema Program hiyo iliyoanzishwa na Mgodi wa kuwajengea uwezo Wazawa na kuwapatia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Mgodi huo, zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko ya vijana kulilia kukosa ajira ndani ya Mgodi.
Aidha, Msimamizi wa vijiji 14 ambavyo vinauzunguka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Joseph Rubega, akielezea namna Mgodi huo unavyotoa fursa za ajira kwa Wazawa na kujikwamua kiuchumi.
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Bushing'we ambayo inajengwa na Wazawa kupitia fursa za Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa thamani ya Sh.miloni 88 fedha ambazo siyo za CSR.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464