Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
SERIKALI mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania(TFS)Kanda ya Magharibi, wamejadili na kupanga mikakati ya kutekeleza maamuzi ya Baraza la Mawaziri Nane Kisekta juu ya kutatua Mgogoro wa Hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani Shinyanga na wananchi ambao wamevamia hifadhi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Kikao hicho kimefanyika leo Juni 26, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kujadili namna ya kuendesha zoezi la kuondoa wananchi waliovamia hifadhi na kuhamishwa katika eneo jingine ambalo limemengwa ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili Makazi lenye ukubwa wa Hekta 3,726.98
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mhifadhi Mkuu daraja la Pili Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS)Kanda ya Magharibi Lucas Nyambala, akiwasilisha maelekezo ya Baraza la Mawaziri Nane Kisekta kuhusu utatuzi wa Migogoro ya Ardhi kati ya Hifadhi ya Msitu wa Nindo na Wananchi katika vijiji ambavyo vimevamia eneo hilo la hifadhi, kwamba litatuliwe kwa maridhiano.
Mhifadhi Mkuu daraja la Pili Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS)Kanda ya Magharibi Lucas Nyambala,
Amesema mwaka juzi Mawaziri Nane walifanya ziara maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kutatua Migogoro ya Ardhi kati ya Hifadhi na Vijiji, na mwaka jana wakiwa mkoani Shinyanga walitoa maelekezo juu ya kutatua Mgogoro wa Hifadhi ya Nindo na Wananchi wa vijijini Sita wilayani Shinyanga ambao wamevamia eneo hilo na kufanya makazi.
Kamishina Msaidizi Mwandamizi TFS Kanda ya Magharibi Ebratino Mgiye akizungumza kwenye kikao hicho.
Amesema eneo hilo la Hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani Shinyanga. lilitambuliwa kisheria na kutangazwa na Gazeti la Serikali No 10 mwaka 1958, na lilikuwa na ukubwa wa Hekta 27,446, lakini baada ya kuvamiwa na wananchi ukubwa wake umesalia hekta 10,969.98.
“Vijiji Sita ambavyo vimevamia eneo la Hifadhi ya Msitu wa Nindo ni Ng’homango, Mwabundala, Lyamidati, Kadoto, Mwajiji na Buzinza, ambapo wananchi wamemiliki ardhi zaidi ya Hekali 2,000 hadi 5,000,”amesema Nyambala.
Aidha, amesema katika utatuzi wa Mgogoro huo Serikali chini ya Rais Samia kupitia Baraza hilo la Mawaziri Nane, ndani ya Hifadhi hiyo ya Msitu wa Nindo limemegwa eneo lenye ukubwa wa Hekta 3,726 kwa ajili ya makazi ya wananchi, na wanapaswa kupisha maeneo mengine ya hifadhi na kuishi katika eneo ambalo limetengwa kwa ajili yao, huku Hekta 7,243 zikibaki kusimamiwa na TFS.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amempongeza Rais Samia kwa kutenga eneo ndani ya hifadhi hiyo ya Msitu wa Nindo kwa ajili ya makazi ya wananchi, huku akiwasihi wananchi ambao wanapaswa kupisha maeneo mengine ya hifadhi waridhie kuondoka na kuishi eneo ambalo limetengwa kwa ajili yao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Nao wajumbe wa kikao hicho wakitoa maoni yao kwenye majadiliano, wamesema kabla ya wananchi kuanza kuhamishwa wapewe elimu kwanza juu ya kupisha eneo ambalo limesalia kwa ajili ya hifadhi, na baada ya kupisha maeneo hayo yawekewe alama za mipaka ili kusijitokea uvamizi mwingine.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Kamishina wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Leo Komba akichangia Mada kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akichangia mada kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akichangia Mada kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Diwani wa Iselamagazi Isack Sengerema akichangia Mada kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akichangia mada kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Diwani wa Lyamidati Veronica Nduta akichangia mada kwenye kikao hicho.
kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464