Ofisi ya Taifa ya ukaguzi yatoa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
OFISI ya Taifa ya ukaguzi imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga juu ya majukumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pamoja na kuripoti habari za ukaguzi kwa ufasaha.
Mgeni Rasmi Anna Massanja ambaye ni Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (AAG) akifungua mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Juni 28, 2023 Mjini Shinyanga.
Mgeni Rasmi Anna Masanja akizungumza kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa waandishi wa habari kuwajengea uwezo namna wanavyofanya shughuli za kikaguzi, ili kuripoti habari zao kwa usahihi bila ya upotoshaji.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Shinyanga Patric Lugisi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
“Tunatambua na kuheshimu mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari katika kuelimisha umma, jambo ambalo limesababisha jamii kuendelea kufahamu na kutambua umuhimu wa Ofisi ya (CAG),”amesema Anna.
“Hii siyo mara ya kwanza Ofisi ya Taifa ya ukaguzi kufanya mafunzo ya aina hii kwa Waandishi habari, kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukiendesha mafunzo ya aina mbalimbali kwa Wahariri na Waandishi wa habari kutoka maeneo mengine na mafunzo haya yatakuwa endelevu,”ameongeza.
Mafunzo yakiendelea.
Katika hatua nyingine amewahimiza Waandishi wa habari wawe na uelewa mkubwa wa masuala ya fedha za umma, na kujifunza kuhusu mifumo ya bajeti, taratibu za manunuzi na sheria zinazosimamia matumizi ya fedha za umma, ujuzi ambao utawawezesha kufanya uchambuzi bora na kutoa taarifa sahihi kwa umma.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa waandishi habari kutambua kwa upana shughuli za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa nje wa hesabu za Serikali, ili kuisaidia jamii kupata uelewa kupitia habari na kufuatilia rasilimali zao kwa ajili ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Shinyanga Greyson Kakuru.
“Naipongeza Ofisi ya Taifa ya ukaguzi kwa kutupatia mafunzo haya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kwa mara ya kwanza, ambayo yametujengea uwezo namna ya kuripoti habari zetu kwa ufanisi, na kuibua habari za usimamizi wa fedha”anasema Kakuru.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Aidha,kwenye mafunzo hayo zimefundishwa mada mbalimbali ikiwamo ya Sheria na kanuni zinazosimamia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Aina mbalimbali ya Ripoti za Mdhibiti na Misingi ya Mawasiliano na habari baina ya Ofisi ya CAG na vyombo vya habari.
Tazama picha hapa chini za mafunzo hayo👇👇
Mkurugenzi wa huduma na sheria Elieshi Saidimu,akitoa mafunzo juu ya mada ya Sheria na kanuni zinazosimamia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.
Hagai Maleko akitoa mafunzo ya aina mbalimbali ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Focus Mauki, akitoa mafunzo ya Misingi ya Mawasiliano na Habari, baina ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga Greyson Kakuru akifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo kutoka Ofisi ya Taifa ya ukaguzi.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo kutoka Ofisi ya Taifa ya ukaguzi.
Mafunzo yakiendelea.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Mafunzo yakiendelea
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Picha ya pamoja ikipigwa.