WAZIRI UMMY MWALIMU AWAPONGEZA DKT. YOTI NA BI. SHALINI KWA KUIMARISHA MIFUMO SEKTA YA AFYA.
Na. Mwandishi wetu – WAF
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo ameagana rasmi na kuwapa pongezi zao Mwakilishi wa UNICEF Bi. Shalini Bahuguna pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WHO Dkt. Zablon Yoti aliyewakilishwa na Bw. Maximilian Mapunda ambao walimaliza muda wao wa kutumikia nafasi hizo hapa Nchini.
Waziri Ummy ametoa pongezi hizo mapema Leo katika hafla fupi ya kuwaaga viongozi hao katika ukumbi wa Serena Hotel, jijini Dar es Salaam.
“Nawashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri mliyoifanya hapa nchini kwa kuendelea kuimarisha mifumo katika sekta ya Afya hususani maeneo ya upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo kwa watoto na masuala ya usafi na lishe”. Amesema Waziri Ummy
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Bi. Shalini Bahuguna ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye mashirika ya kimataifa ikiwemo UNICEF NA WHO.
Naye Bw. Maximilian Mapunda aliyemuwakilisha Mwakilishi mkazi wa WHO Dkt. Zablon Yoti ameiwashukuru Wizara ya Afya kwa ushirikiano walioutoa wakati wa muda wake na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya.