Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amehitimisha ziara yake ya kuhudhuria vikao Maalumu vya Baraza la Madiwani katika Halmashauri tatu wilayani Kahama vya kujadili hoja za CAG.
Mabaraza aliyohudhuria ni Baraza la Manispaa ya Kahama, Ushetu na kuhitimisha katika Halmashauri ya Msalala ambapo madiwani walikuwa wakijadili
mapendekezo kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023.
Akiongea wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kuhudhuria vikao kwenye Mabaraza hayo katika Halmashauri ya Msalala Mhe. Mndeme amezipongeza Halmashauri zote tatu namna zilivyopambana kujibu na kufuta hoja.
Amesema, madiwani pamoja na watumishi wote wa Halmashuri wakishikamana kwa pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kuzingatia misingi, Sheria, Kanuni na taratibu za kazi pamoja na kutanguliza uzalendo, kuna uwezekano kabisa wa kuondoa hoja zote.