SHIRIKA LA REDESO LAZINDUA MRADI WA KUIMARISHA USTAHIMILIVU WA KIPATO


Na Sumai Salumu,KISHAPU

Shirika lisilokuwa la kiserikali REDESO wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga limezindua mradi wa Kuimarisha ustahimilivu wa kipato na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye mnyororo wa thamani wa zao la mkonge Mkoani Shinyanga ambapo utakuwa katika kata Tano Kishapu,Uchunga,Shagihilu,Lagana na Negezi.

Uzinduzi huo umefanyika leo june 2023 katika ofsi za Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ambapo Meneja mkuu wa kitengo Cha kutafuta fedha za miradi Bi.Christina John amesema kuwa Mradi huo ni wa miaka 3 na bajeti yake ni Tsh.367,718,000 ambapo Care International imepata ufadhiri wa fedha kutoka kwa Tanzania Fund Friends.

Hata hivyo meneja huyo amesema lengo haswa la kuleta mradi huo wilayani Kishapu ni kuongeza uzalishaji,lishe,kuongeza kipato,uhimilivu katika kukabiliana na mabadiliko tabianchi,usawa,ushawishi na upatikanaji wa soko la unakula wa zao la mkonge kupitia wakulima wadogo na yote hayo ni ili kurudisha hali ya mwanzo ya uzalishaji kabla ya kanga la Uviko-19.

Aidha akizungumza kwenye uzinduzi huo meneja mradi REDESO Kishapu Bw.Charles Buregeya amesema kuwa wanufaika wa mradi 70%ni wanawake na 30% wanaume ,wanufaika wa moja kwa moja katika mradi huo ni 1,200 na wasio wa moja kwa moja ni 6000 ambapo kunamradi wa zao la mkonge,ufugaji kuku Aina ya saso,bustani za mbogamboga kwani hii itawasaidia kupata fedha za kuendesha maisha wakati wakisubilia miaka 3 ya uvunaji mkonge.

Hata hivyo Buregeya ameongeza kuwa Hadi hii Leo tayari wameanza utekelezaji wa mradi wa kuku pamoja na ukarabati na ujengaji wa vitalu nyumba(green houses) 2 katika jijini Cha mihama na lagana ambapo wanufaika wamepanda nyanya Huku vifaranga vya kuku vikiwa na zaidi ya mwezi mmoja.

Kwa upande wake mdau wa mradi wa kuku kutokea kata ya Ukenyenge Bi.Rehema Ally amesema kuwa mradi wa ufugaji kuku ni mzuri kwani amesomesha watoto wake 7 kwenye shule binafsi wakati akiishi na kuku na sasa mradi huu utamasaidia kufuga kuku kibiashara.

Aida Bi. Annastazia Christopher ni mdau wa kuongeza thamani (usinga) kutokea kata ya Isoso licha ya kuipongeza care kwa kuwa mfadhiri wa REDESO amesema kuwa kutafutiwa kwa masoko ya bidhaa zao itakuwa mkombozi kwao kwani itawafanya wanawake wengine kukimbilia fursa ya utengenezaji wa bidhaa hizo.

Kwa upande wake mtendaji wa kata ya uchunga Bw.Ignas Mpiluka amesema kuwa atahakikisha anafuatilia vema mradi huo katika vijiji vyote vya mradi wake Huku akiahidi kuendelea kutoka elimu ya mikopo ya fedha kwa wanakikundi yenye liba nafuu kwa lengo la kuhakikisha uchumi wa mtu mmojammoja na kata unaongezeka.

Mwakilishi kutoka ofsi ya mkuu wa mkoa ambaye pia ni afisa maendeleo Bi.Rehema Edson amewapongeza Care kuwa mfadhiri ndani ya mkoa wa Shinyanga na ametoa rai kwa watumishi wa ngazi ya wilaya,kata na vijiji kuhakikisha wanakuwa wafuatiriaaji maeneo yote ya mradi kwa ajili ya kufikia Kishapu yenye hali nzuri ya kiafya na kiuchumi.

Hata hivyo mradi huuShirika la Care INTERNATIONAL limekusudia kulenga kundi la wanawake kuwa wanufaika wakubwa kutokana na Mila na desturi kandamizi zinazowafanya wanawake wawe nyuma kuchangamkia fursa za maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464