RC MNDEME APIGA MARUFUKU UUZWAJI WA CHAKULA NJE, AAGIZA KILA HALMASHAURI KUWA NA GHALA KWA AJILI YA CHAKULA CHA AKIBA

RC MNDEME APIGA MARUFUKU UUZWAJI WA CHAKULA NJE, AAGIZA KILA HALMASHAURI KUWA NA GHALA KWA AJILI YA CHAKULA CHA AKIBA.

Na. Shinyanga RS.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amepiga marufuku kwa yeyote kutoa na kuuza chakula katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote kuhakikisha wanakuwa na ghala la chakula kwa ajili ya akiba iwapo inatokea lolote kwa wananchi wa eneo hilo kuweza kujikwmua.

Hayo ameyasema leo tarehe 15 Juni, 2023 wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, maafisa Uhamiaji wa Wilaya zote, maafisa ugani kutoka katika Halmashauri zote wakati akipokea taarifa ya hali ya usalama wa chakula kutoka katika Wikaya na Halmashauri zote katika kikao kilichofanyika ofisini kwake.

Mhe. Mndeme amema kuwa, kumekuwa na tabia ya wakulima kuuza chakula chote mpaka cha akiba kwa wafanyabiashara wanaosafirosha kwenda Nchi za nje jambo ambalo linapelekea kuwa na upungufu wa chakula wa wananchi nahivyo kuifanya Serikali kuwasaidia jambo ambalo likidhibitiwa mapema laweza kuokoa adha hiyo huku akiitaja Manispaa ya Kahama kuwa ni kinara wa uuzaji wa mazao nje ya nchi jambo ambalo limempelekea kuitisha kikao hicho na kuwataka maafisa Uhamiaji kuacha kqbisa kutoa bibaoi kwa wageni yoka nje ambao wananunua mazo hayo.

"Nitoe wito kwa maafisa uhamiaji wote kutoka kila Wilaya kuacha mara moja kuyoa vibali kwa wageni amnao wamekuwa wakinunua chakula kwa wananchi hasa katika Manispaa ya Kahama ambapo imeonekana kama ndiyo kituo kikuu cha ununuzi wa chakula kutoka kwa wananchi, na pia niwaagize Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote kuhakikisha mnakuwa na ghala kwa ajili ya chakula cha akiba ili inapotokea upunhufu wowote akiba hiyo iweze kutumika kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wa eneo husika," alisema Mhe. Mndeme.

Kwa upande wao wajumbe wa kikao hicho walipokea na kumuahidi Mhe. Mndeme kuwa watakwenda kutekeleza maelekezo yote aliuowapatia katika maeneo yao.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464