WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE YA SEKONDARI WIGEHE WATEMBELEA SHULE YAO,WAKOSHWA NA UWEKEKEZAJI WA CHERISH FOUNDATION


Umoja wa wanafunzi waliosoma miaka tofauti katika Shule ya Sekondari Wigehe,leo Jumamosi Juni 24,2023 wametembelea shule hiyo na kupongeza mabadiliko yaliyopo.

Akiongea katika kikao kilichofanyika Shuleni hapo Mwenyekiti wa Umoja huo Mayunga James amesema wamefurahi kuona Shule yao imeanza kuwa na mabadiliko makubwa baada ya Cherish Foundation kuanza uwekezaji wa kutoa Elimu ya kidato cha Tano na Sita.

James amesema kuwa Umoja wao wa Ex Wisesco huwa wanatembelea shuleni hapo na kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kupaka rangi na kuboresha miundo mbinu mbalimbali.

Sambamba na hayo James amesema kuwa wanafunzi waliosoma Wigehe sekondari watatoa ushirikiano kwa mwekezaji Cherish Foundation pamoja na Chama Cha Mapinduzi kwa jumla.

Nao baadhi ya Wanafunzi waliosoma shuleni hapo Subira Aoko na Isack Manga wamesema kuwa wamefurahi kuona shule yao inarudi katika ubora na kuahidi kuwa mabalozi wakubwa wa shule Hiyo.

Nao baadhi ya Walimu waliostaafu waliokuwa wanafundisha Shule Hiyo akiwemo mwalimu Kushoka Bundala na Lucas Mapalala wamewapongeza wanafunzi waliosoma shule ya Wigehe kutembele Shule Hiyo mara kwa mara na kufanya maboresho katika Shule hiyo huku wakiwapongeza Cherish Foundation kwa kuanza kutoa Elimu ya kidato cha Tano na Sita katika Shule hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Wigehe kutoka Cherish Foundation Mwalimu Charles amewashukuru wanafunzi waliosoma shuleni hapo kutembelea shule hiyo na kueleza malengo Yao ikiwa ni pamoja na Shule ya Wigehe kutoa Mwanafunzi bora wa sayansi nchini Tanzania na kutoa Elimu bora inayoendana na soko la ajira kwa wahitimu.

Umoja wa wanafunzi waliosoma Wigehe sekondari (Ex Wisesco) una Wanachama 173 walio hai wenye utaratibu wa kutembelea Shule ya Wigehe Kila mwaka.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464