Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.
Na mwandishi wetu.
Serikali
ya mkoa wa Shinyanga imezindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya sheria ili kuweza
kukabiliana na changamoto za ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi na ndoa
na masuala ya mirathi katika familia.
Uzinduzi
wa Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Kisheria,umefanyika leo juni 11,2023 katika manispaa ya Shinyanga
ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.Christina Mndeme kwa ajili ya kuhamasisha
wananchi kuweza kupata elimu ya sheria ili
kutambua haki,usawa na maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Kampeni ya msaada wa kisheria Mama Samia ina dhumuni la kutoa elimu bure ya sheria kwa wakazi wa mkoa wa huu kwa siku 10 ili
kufikia wananchi wote kwa lengo kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu
kwa jamii hususan haki za wanawake na watoto,Kuimarisha huduma ya ushauri wa
kisheria kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na kuongeza uelewa kwa wananchi
kuhusu elimu ya sheria kwa umma, masuala ya haki na wajibu na misingi ya
utawala bora.
Mndeme
amesema Kampeni hii itasaidia kuondoa kadhia mbalimbali zinazonyima haki za wanawake
na watoto mkoa hapa na aliomba jeshi la polisi kuhakikisha linashughulia kesi za mimba na ndoa za utotoni na ubakaji zilizo na muda mrefu kwa watuhumiwa
kutofikishwa mahakamani na kutaka umakini juu ya dhamana.
“Jeshi
la polisi liwe makini na dhamana za watuhumiwa wa masuala ya ukatili wa kijinsia,
Mtu amebaka mtoto wake na unampa dhamana arudi nyumbani kwake tena,Ni vema
tuangalie hizi dhamana”,amesema Mndeme.
Aidha,Mndeme
alitoa wito kwa viongozi wote ngazi ya kata kwa mkoa wa shinyanga kutenga vyumba maalum kwa
ajili ya kurahisisha huduma ya msaada wa kisheria kwa siku zilizopangwa kwa utoaji
wa elimu.
“Ni wajibu wetu watendaji wa serikali kuhahakisha
wananchi wote wanafikiwa na huduma hii kwa ngazi zote”,amesema Mndeme.
Kwa
upande wake,Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga,Donald Magesa
amesema,wako tayari kuruhu ofisi za ccm ngazi ya kata kutumika kutoa huduma kwa
wananchi wote bila ubaguzi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM katika ibara
namba mia moja kumi na tisa na ishirini.
Naye,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Pauline Philipo Gekul, aliomba watendaji wa
serikali kuhamasisha wananchi kuweza kupata huduma kwani itasaidia kuondoa
migogoro ndani ya jamii na kupata kazi nyepesi juu majukumu yao.
Nao
wabunge wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Christina Mzava na Mhe.Santiel Kirumba,wamesema
kampeni hii itasaidia kuiondoa shinyanga kama kinara wa matukio ya ukatili wa
kijinsia,migogoro ya ardhi na kusaidia wananchi kupata msaada wa sheria bure.
“Ni wakati wa kupaza sauti na kufuatilia haki za
ardhi kwa wanawake na hali ya utekelezaji wa watoto”Anasema Santiel.
Meneja Rasilimali na Mawasiliano kutoka Legal services Facility(LSF), Jane
Matinde,alisema Kampeni itasaidia kutatua migogoro ndani ya jamii na inalenga
kusaidia watanzania wanyonge dhidi ya gharama za kisheria.
Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama
Samia Legal Aid Campaign”, John Shija ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za msaada
wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga ameitaja migogoro inayoongoza mkoani Shinyanga
kuwa ni ardhi, ndoa, kazi na matunzo ya watoto hivyo kampeni hiyo itakuwa
sehemu ya suluhisho la kumaliza migogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga. Wa kwanza Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za msaada wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Rasilimali na Mawasiliano kutoka Legal Services Facility (LSF), Jane Matinde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakicheza wakati Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi na wananchi wakicheza wakati Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Viongozi wa CCM na vijana wa hamasa UVCCM wakicheza wakati Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Moja ya bango wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakicheza na vijana kutoka NACOPHA wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwasili katika uwanja wa Sabasaba kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitembelea mabanda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Wananchi wakiendelea kupata huduma kwenye Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul.
Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul.
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Picha mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464