Mjumbe wa mkutano mkuu wazazi Taifa Edwin Kenyenge akizungumza kwenye baraza la wazazi wilaya ya Shinyanga mjini
Suzy Luhende, Shinyanga Press Blog
Mjumbe wa mkutano mkuu wazazi Taifa Taifa Edwin Nyakanyenge ameipongeza Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kufanya ziara ya kuimalisha Chama na Jumuiya zake pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya CCM,katika kata 17 za wilaya hiyo.
Pongezi hizo amezitoa leo alipokuwa mgeni wa kikao cha baraza la Jumuiya hiyo kilichofanyika leo june 17, 2023 ambapo amesema Jumuiya ya wazazi Shinyanga imefanya kazi kubwa tofauti na Jumuiya za wilaya zingine za mkoa wa Shinyanga.
Nyakanyenge amesema kutokana na kazi kubwa walioifanya amewaomba waendelee kupambana zaidi ili kuhakikishanafadi zote ambazo zipo wazi zijazwe ili kazi iweze kuendelea kwasi zaidi na kuhakikisha mwaka 2025 ushindi wa CCM unapatikana kwa kishindo.
"Niwapongeze sana kwa kazi mliyoifanya ni kubwa sana kutembelea kata 17 si mchezo, hivyo niwaombe mjiandae na kongamano kubwa la mkoa wa Shinyanga, na niombe nafasi zilizo wazi zijazwe haraka na viongozi ambao hawawajibiki ipasavyo waachie nafasi ili tuweze kuweka viongozi wanaoweza kusimama na sisi, kwani Rais wetu mama Samia anatutegemea sisi"amesema Nyakanyenge.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko amewataka wajumbe wapendane wawe na umoja ili kuweza kufanya mambo mazuri ya Jumuiya na Chama kwani bila upendo hakuna kazi nzuri itakayofanyika.
"Niwaombe ndugu zangu mpendane uchaguzi umeisha na sisi tunatakiwa kufanya kazi kwa pamoja, tunatakiwa tushikamane na viongozi wetu ambao tayari tuliwapa dhamana ya kukitumikia Chama,"amesema Mrindoko.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Okuku Obata alishauri waendelee kufanya kazi ili chama kiendelee kusonga mbele aliwapongeza kwa kumaliza ziara yakukagua miradi mbalimbali ya wilaya, hivyo kuwaomba waendelee na nhuvu hiyo hiyo.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi wakati akisoma taarifa yake mbele ya mjumbe wa mkutano mkuu Taifa amesema kamati ya utekelezaji imefanya ziara katika kata zote 17 za wilaya ya Shinyanga mjini na kusababisha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali.
"Ziara hiyo ilikuwa ni ya kuimarisha Chama na Jumuiya zake, ambapo tumefanikiwa kutatua migogoro mbalimbali katika kata zilizokuwa na migogoro,tumekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali, tumehamasisha viongozi kusajili wanachama wake na kutoa ada kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kuongeza wanachama na jumuiya zake"amesema Kibabi.
Kibabi amesema katika kipindi cha mwezi January hadi June mwaka 2023 wamefanikiwa kuingiza wanachama wapya 312, na wanaelekea kuanzisha mradi wa ufyatuaji wa tofali aina ya block na mpaka sasa mradi huo umetumia kiasi cha zaidi ya Sh 5.3 milioni.
"Pia tayari tuna viwanja 10 kumi vipya kwa ngazi ya wilaya viwili, viwanja nane kwa kata ya Ibadakuli, Ibinzamata,Kizumbi,Chibe, Ndembezi, na Ngokolo,ambapo tumewaagiza kila kata ifikapo mwezi Desemba iwe imepata kiwanja au shamba au kitega uchuni chochote ili kila ngazi ijitegemee kiuchumi"amesema Kibabi.
Amesema katika ziara hiyo ya kukagua miradi wamekuta baadhi ya miradi inayotekelezwa na serikali ipo chini ya kiwango ambayo imetumia tofari za kumomonyoka mfano shule ya msingi ya Msufini kata ya Ndala.
"Pia tumefika kwa baadhi ya shule ikiwemo shule ya Mwamalili Sekondari tukakuta utoro wa wanafunzi 40 hawafiki shule kwa wakati mmoja ambayo ni kero, hivyo wazazi walezi wanatakiwa wawajibike kwa hilo"amesema Kibabi.
"Lengo letu kubwa tunataka jumuia ijengwe kuanzia chini mpaka juu, hivyo nitashirikiana na viongozi wenzangu mpaka kieleweke na kuhakikisha tunafanya kazi vizuri katika kutekeleza majukumu ya jumuiya yetu na Chama.
Baadhi ya viongozi akiwemo katibu wa Jumuiya ya wazazi kata ya Kambarage Zakia Bashiri, na Gabriel Swila, katibu wa kata Kitangili na Sheka Ngusa kata ya Kolandoto wameishukuru kamati ya Utekelezaji kufanya ziara kwani imeamsha uhai wa Chama na Jumuiya zake, na kuwataka waendelee kufanya kazi.
Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa Edwin Nyakanyenge akiingia kwenye kikao cha baraza la Jumuiya ya wazazi Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko akifurahia baada ya kukaribishwa kuzungumza kwenye kikao cha baraza hilo
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Jumuia hiyo
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Jumuia hiyo
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi akisoma taarifa mbele ya Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa Edwin NkenyengeKatibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Jumuia hiyo
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi mkoa wa Shinyanga Obata Okuku akizungumza kwenye baraza la wazazi wilaya ya Shinyanga mjini
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Richard Kapaya akizungumza
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mary Makamba akizungumza Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Zulfa Dali akizungumza
Viongozi baada ya kumaliza kikao wakitoka
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi Shinyanga mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa Mkutano mkuu wazazi Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Viongozi wakiwa kwenye kikao cha baraza la Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga
Wakicheza baada ya mjumbe wa mkutano mkuu Taifa Jumuiya ya Wazazi kufika
Msanii wa kizazi kipya wa Shinyanga mjini Nyasani akitoa burudani baada ya kuingia mjumbe wa mkutono mkuu Taifa Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Wajumbe wakimsikiliza mjumbe wa mkutano mkuu Taifa
Wajumbe wakimsikiliza mjumbe wa mkutano mkuu Taifa