Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya siasa ya CCM Mkoani humo.
Na Halima Khoya,Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa kufanya mikutano ya hadhara kwenye mitaa yao ili kusikiliza changamoto za wananchi kuelekea uchaguzi ujao 2024 kwa ngazi ya Mitaa.
Maagizo hayo yametolewa leo June 19 2023 katika ziara ya kikazi ya Kamati ya siasa ya CCM iliyofanyika kwa lengo la kukutana na Mabalozi Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga.
Mlolwa amesema kuwa kuelekea uchaguzi ujao 2024 viongozi wa Serikali za mitaa wanapaswa kuwajibika kwa wananchi wao kwa kutembelea na kutatua changamoto sambamba na kujionea maendeleo ya miradi mbali mbali ili kujenga uaminifu kwa wapiga kura wao.
“Wenyeviti wa matawi na Kata nendeni mkakague miradi,uhai wa chama na changamoto za wananchi ili ikifika wakati wa uchaguzi mgombea unakuwa unajieleza mwenyewe kwa wananchi wako,je wanakukubali?,wanakuamini?,unatatua changamoto zao?,hiyo itasaidia kupita kwa wepesi”, amesema Mlolwa.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amesema baada ya vikao kumalizika kuna shughuli za uhamasishaji kwa wananchi ambapo amemtaka katibu wa tawi na katibu wa kata kuwatafuta mabalozi kwaajili ya kufanya kikao nao.
Wakizungumza kwa niaba ya Wajumbe,Haji Mtaki na Kulthum Ally wakati wa kuuliza maswali na kueleza changamoto ya utolewaji wa huduma za kiafya kwenye hospitali ya Rufaa Mwawaza na kudai kuwa kumekua na baadhi ya watoa huduma katika hospitali hiyo wanaoshindwa kutoa huduma ipasavyo.
Akitoa majibu kwa wajumbe hao,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Shinyanga,Mabala Mlolwa amewaasa wananchi kuwa wavumilivu kwani serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani imetoa fedha kwenye miradi mingi na kwamba itachukua muda kukamilisha changamoto hizo.
“Nizibebe changamoto zenu kama zilivo na nitazifikisha kwenye ngazi ya juu,kuweni wavumilivu nitazisuluhisha kwa kipindi hichi”,ameongeza.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.
Wajumbe na Mabalozi wa chama cha mapinduzi kata ya Mjini wakiendelea na kikao na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa Shinyanga.
kikao kikiendelea katika ofisi ya chama cha mapinduzi kata ya mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akiendelea na kikao kwenye ofisi ya soko la nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza kwenye kikao cha kamati ya siasa (CCM Mkoa).
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza akiwa kwenye kikao cha kamati ya siasa(CCM Mkoa).
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akitembelea soko la Nguzo nane wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya siasa ya CCM Mkoani humo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464