CHAMA cha
wafanyabiashara,viwanda na kilimo –Tanzania(TCCIA) kimepata mwenyekiti mpya
Jonathan Manyama aliyechaguliwa kwa kishindo na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa
huku akieleza wamuamini katika kuendeleza
mabadiliko zaidi kwenye chama hicho.
Uchaguzi huo umefanyika
leo tarehe 14/06/2023 wilayani
Kahama ambapo mwenyekiti wa kamati ya
uchaguzi Zipora Pangani aliendesha
uchaguzi huo kwa nafasi nane zilihitaji
wagombea.
Pangani amewataja
viongozi waliogombea baada ya kupigiwa kura nakupata ushindi ni nafasi ya
mwenyekiti wa TCCIA mkoa Shinyanga, aliibuka Jonathani Manyama kwa kupewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi cha
miaka minne.
Pia nafasi ya Makamu Mwenyekiti Biashara
amechaguliwa Hatibu Mgeja, Makamu mwenyekiti viwanda amechaguliwa Emanuel
Kidenya na Makamu mwenyekiti kilimo amechaguliwa Nasir Said.
Mjumbe ambaye
anawakilisha kundi la wanawake Taifa ni
Joyce Egina,Mjumbe anayewakilisha vijana
ni Catherine Kaliwa na Mosses Mwanakulya.
Mgeja amesema ametembea nchi za jirani nakuona wafanyabiashara
wa Tanzania bado wana fursa za kujifunza nakupeleka bidhaa zao hivyo jukumu walilompa la kusimamia viwanda litaonekana.
Boniface Ndengo ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya TCCIA Taifa na mwenyekiti
wa TCCIA mkoa wa Mara akiwa mgeni rasmi katika mkutano huo amesema
viongozi wapya waliochaguliwa
waendeleze mahusiano sababu wanakutana na wadau wengi wakiamini hakuna
migogoro.
Ndengo amesema inapotokea migogoro wanatakiwa wasimamie ili kuipa uhai TCCIA na
kuhimiza vikao vya mabaraza ngazi ya wilaya na mkoa vifanyike ili
kujua changamoto.
Ndengo amesema TCCIA wanajukumu la kuwawezesha wafanyabiashara kufika hatua ya kimataifa kwa kukutana mara kwa mara na kubadilishana uzoefu kwa kulinganisha makundi yote ya wafanyabiashara namna ya ufanyaji wa biashara na ubunifu.
Afisa biashara mkoa wa Shinyanga Rose Tungu amesema kuna mabaraza mengi katika mkoa huu wayatumie
kueleza changamoto zao ili ziweze kufika kwenye ngazi ya mkoa na kutatuliwa na kuzishauri
taasisi za kifedha kutoa ushirikiano.
MATUKIO KATIKA PICHA