MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI WAZAZI CCM TAIFA AIPONGEZA JUMUIYA YA WAZAZI SHINYANGA MJINI KUFANYA ZIARA KATA 17 YA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA NA JUMUIYA ZAKE


Mjumbe wa kamati ya utekelezaji  wazazi CCM Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza kwenye kikao cha baraza la Jumuiya ya wazazi Shinyanga mjini

Suzy Luhende, Shinyanga Press Blog

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi CCM Taifa Edwin Nyakanyenge ameipongeza Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kufanya ziara ya kuimalisha Chama na Jumuiya zake pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya CCM,katika kata 17 za wilaya hiyo.

Pongezi hizo amezitoa leo wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha baraza la Jumuiya hiyo kilichofanyika leo june 17, 2023 ambapo amesema Jumuiya ya wazazi Shinyanga imefanya kazi kubwa tofauti na Jumuiya za wilaya zingine za mkoa wa Shinyanga.

Nyakanyenge amesema kutokana na kazi kubwa walioifanya amewaomba waendelee kupambana zaidi ili kuhakikisha nafasi zote ambazo zipo wazi zijazwe na kazi iweze kuendelea kwasi zaidi na kuhakikisha mwaka 2025 ushindi wa CCM unapatikana kwa kishindo.

"Niwapongeze sana kwa kazi mliyoifanya kwani ni kubwa sana kutembelea kata 17 si mchezo, hivyo niwaombe mjiandae na kongamano kubwa la mkoa wa Shinyanga, na niombe nafasi zilizo wazi zijazwe haraka na viongozi ambao hawaajibiki ipasavyo waachie nafasi ili tuweze kuweka viongozi wanaoweza kusimama na sisi, kwani Rais wetu mama Samia anatutegemea sisi"amesema Nyakanyenge.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko amewataka wajumbe wapendane wawe na umoja ili kuweza kufanya mambo mazuri ya Jumuiya na Chama, kwani bila upendo hakuna kazi nzuri itakayofanyika.

"Niwaombe ndugu zangu mpendane uchaguzi umeisha na sisi tunatakiwa kufanya kazi kwa pamoja, tunatakiwa tushikamane na viongozi wetu ambao tayari tuliwapa dhamana ya kukitumikia Chama,"amesema Mrindoko.

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Okuku Obata alishauri waendelee kufanya kazi ili chama kiendelee kusonga mbele na aliwapongeza kwa kumaliza ziara yakukagua miradi mbalimbali ya wilaya na kuimarisha Chama na Jumuiya zake, hivyo kuwaomba waendelee na nguvu hiyo hiyo.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi wakati akisoma taarifa yake mbele ya mjumbe wa mkutano mkuu Taifa amesema kamati ya utekelezaji imefanya ziara katika kata zote 17 za wilaya ya Shinyanga mjini na kusababisha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali.

"Ziara hiyo ilikuwa ni ya kuimarisha Chama na Jumuiya zake, ambapo tumefanikiwa kutatua migogoro mbalimbali katika kata zilizokuwa na migogoro,tumekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali, tumehamasisha viongozi kusajili wanachama wake na kutoa ada kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kuongeza wanachama na jumuiya zake"amesema Kibabi.

Kibabi amesema katika kipindi cha mwezi January hadi June mwaka 2023 wamefanikiwa kuingiza wanachama wapya 312, na wanaelekea kuanzisha mradi wa ufyatuaji wa tofali aina ya block na mpaka sasa mradi huo umetumia kiasi cha zaidi ya Sh 5.3 milioni.

"Pia tayari tuna viwanja 10  vipya, kwa ngazi ya wilaya viwili, viwanja nane kwa kata ya Ibadakuli, Ibinzamata,Kizumbi,Chibe, Ndembezi, na Ngokolo,ambapo tumewaagiza kila kata ifikapo mwezi Desemba iwe imepata kiwanja au shamba au kitega uchuni chochote ili kila ngazi ijitegemee kiuchumi"amesema Kibabi.

Amesema katika ziara hiyo ya kukagua miradi wamekuta baadhi ya miradi inayotekelezwa na serikali ipo chini ya kiwango ambayo imetumia tofari za kumomonyoka mfano shule ya msingi ya Msufini kata ya Ndala.

"Pia tumefika kwa baadhi ya shule ikiwemo shule ya Mwamalili Sekondari tukakuta utoro wa wanafunzi 40 hawafiki shule kwa wakati mmoja ambayo ni kero kubwa, hivyo wazazi walezi wanatakiwa wawajibike kwa hilo"amesema Kibabi.

"Lengo letu kubwa tunataka jumuia ijengwe kuanzia chini mpaka juu, hivyo nitashirikiana na viongozi wenzangu mpaka kieleweke na kuhakikisha tunafanya kazi vizuri katika kutekeleza majukumu ya jumuiya yetu na Chama,"amesema

Baadhi ya viongozi akiwemo katibu wa Jumuiya ya wazazi kata ya Kambarage Zakia Bashiri, na Gabriel Swila, katibu wa kata ya Kitangili na Sheka Ngusa kata ya Kolandoto wameishukuru kamati ya Utekelezaji kufanya ziara kwani imeamsha uhai wa Chama na Jumuiya zake, na kuwataka waendelee kufanya kazi.

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji  wazazi CCM Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza kwenye kikao cha baraza la Jumuiya ya wazazi Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyangani mjini  Fue Mrindoko akifurahia baada ya kukaribishwa kuzungumza
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga mjini Fue Mrindoko akifurahia baada ya kukaribishwa kuzungumza
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga mjini Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga mjini Dorisi Kibabi akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga mjini Dorisi Kibabi akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM  Shinyanga mjini Dorisi  Kibabi akisoma Taarifa mbele ya Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Taifa
Kazi ikiendelea
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi mkoa wa Shinyanga Obata Okuku akizungumza
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi wilaya ya Shinyanga Daniel Kapaya
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Shinyanga mjini Mary Makamba akizungumza
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Shinyanga mjini Zulfa Dali akizungumza

Viongozi wakimsindikiza mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya   wazazi Taifa baada ya kuzungumza na baraza la wazazi Shinyanga mjini
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi  Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi  Taifa

Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi  Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi  Taifa
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi  Taifa akiwasiri kwenye kikao cha baraza la Jumuiya ya Wazazi
Viongozi wakiwa pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi  Taifa 
Wakifurahia baada ya kuwasili mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa 
Msanii wa kizazi kipya Nyasani akitoa burudani baada ya mgeni rasmi mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa baada ya kuwasili
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa
Wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa
Wajumbe wakimsikiliza mjumbe wa mkutano mkuu Taifa

Wajumbe wakimsikiliza mjumbe wa kamati ya utekelezaji  Taifa
Wajumbe wakimsikiliza mjumbe wa kamati ya utekelezaji  Taifa
Wajumbe wakimsikiliza mjumbe wa kamati ya utekelezaji  Taifa


















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464