TRA-YASHAURI WAFANYA BIASHARA KUJAZA TAARIFA SAHIHI KATIKA MFUMO WA MTANDAO.

TRA-YASHAURI WAFANYA BIASHARA KUJAZA TAARIFA SAHIHI KATIKA MFUMO WA MTANDAO.


Wajumbe wa TCCIA wakimskiliza mtaalam kutoka ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania


Ofisa kutoka Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA)  mkoa kikodi Kahama , Godfrey Pochama akitoa elimu kwa wajumbe wa TCCIA


Afisa biashara mkoa wa  Shinyanga , Rose Tungu amewashauri  TRA  kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara
 

Na Kareny Masasy,

Kahama

WAFANYABIASHARA wilayani Kahama mkoani hapa  wameshauriwa  kutumia mfumo uliopo kwenye mtandao wa kujaza taarifa zao zote ili ziweze kuwa kumbukumbu nzuri pasipo kupoteza haki zao pindi wanapofanyiwa hesabu.

Hayo yamesemwa juni 14,2023 na  Ofisa kutoka Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA)  mkoa kikodi Kahama , Godfrey Pochama  alipokuwa akitoa elimu  kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha wafanyabiashara, viwandani na kilimo (TCCIA)

Pochama amesema  madhumuni ya kutoa elimu  kwa wafanyabiashara  ni  kuwaeleza  namna ya kuwasilisha rekodi zao   na risiti zilizokosewa kwani imekuwa changamoto kipindi cha kufanya ukaguzi kupata taarifa.

Pochama amesema  upo mfumo  mpya ulioanzishwa wa  huduma kwa mlipa kodi  ambao umekuwa ukirahisisha kutuma rekodi zao nakurekebisha rsisiti zilizokosewa kwa urahisi.

Afisa elimu kwa mlipakodi kutoka TRA  ,Aniceth  Ndailagije amesema  mfumo umeboreshwa zaidi juu ya uwasilishwaji wa ritani  kwani wafanyabiashara walikuwa wakija moja kwa moja kwenye ofisi lakini sasa wana jaza taarifa huku huko waliko bila usubufu.

Afisa biashara mkoa wa  Shinyanga , Rose Tungu amewashauri  TRA  kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara  ili waweze kutambua zaidi mfumo  nakuondoa  kuibuka kwa migogoro.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo  akiwemo Joyce Egina ambaye ni mchimbaji mdogo wa dhahabu amesema TRA iendelee kutoa elimu hasa upande wa wachimbaji wadogo kwani  bado hawaelewi

 

 

 

 

 

 

 

 


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464