UVCCM SHINYANGA MJINI WAPIGWA MSASA, MWENYEKITI AWAOMBA WALIOPEWA DHAMANA NA CCM WAWAKUMBUKE VIJANA


Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga Jonathan Madete akizungumza kwenye semina elekezi iliyofanyika Shinyanga mjini

Suzy Luhende, Shinyanga press blog

Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga Jonathan Madete amewaomba viongozi waliopewa dhamana na Chama Cha Mapinduzi CCM kuwakumbuka vijana wa jumuia hiyo kwani toka uchaguzi upite wamesahaulika.

Agizo hilo amelitoa jana kwenye semina elekezi ya kuimarisha vijana wa UVCCM Shinyanga mjini, ambapo amewataka viongozi wote wanaopewa dhamana na CCM waweze kusaidia jumuia ya vijana pale inapokuwa na uhitaji wa kufanya shughuli mbalimbali za kichama, ambapo semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini

Madete amesema vijana wa Chama Cha Mapinduzi wamesahaulika kwani wamekuwa wakifanya kazi nyingi za kuwasaidia viongozi mbalimbali nyakati za uchaguzi, lakini wanapohitaji msaada wakati wa kufanya vikao hawasaidiwi, hali ambayo wamewaomba viongozi hao kubadilika.

"Sisi vijana tumesahaulika sana kuna watu wanatuchukulia powa, ifike mahali mtu aliyepewa dhamana na CCM akumbuke fadhila alizofanyiwa na vijana, hali hii imetufanya tufikilie sisi vijana kujitathimini mwaka 2024, kwani tukiwa viongozi wanatokana na Jumuiya ya vijana lazima tutasaidia vijana wenzetu"amesema Madete.


"Ifike mahali na sisi tulipwe stahiki zetu, jumuiya ilipwe thamani inayotakiwa kupewa sio kwamba sisi imekuwa kazi yetu ni kutafuta kura na kuishia hapo mahusiano ya viongozi tuliowatafutia kura, tuthaminiwe nasi pale tunapokuwa na shughuli zetu za kichama jamani inasikitisha sana, hivyo naahidi nitasimama na umoja wa vijana asubuhi mpaka jioni, katika kuhakikisha Chama kinasonga mbele"ameongeza Madete.

Aidha Madete ameiomba serikali iweze kuwakopesha vijana mikopo kwa kupitia silimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya wanawake, watu wenye ulemavu na vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi nakuacha kuwa tegemezi.

Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amesema toka aingie madarakani hajaona maombi ya vijana wa CCM, ya kuomba mkopo, hivyo amewasisitiza wajiunge makundi ili waweze kukopesheka waweze kufanya biashara ili kuhakikisha wanainuka kiuchumi na kuinua Taifa.

"Niwaombe vijana wangu mchangamkie fursa ili muweze kupata mikopo ila cha msingi mzingatie kurejesha kwa sababu hizi fedha ni za watu wote mnaporudisha na wengine waweze kupatiwa, hivi karibuni tulisitisha mikopo ili watu waweze kurejesha lakini tumeshasnza kuweka mambo vizuri ili walioomba waweze kupatiwa,"amesema Masumbuko


Kwa upande wake mgeni rasimi wa semina hiyo mjumbe wa baraza jumuia ya vijana Taifa Monalisa Daniel Fausitine amewataka vijana kuyatekeleza yote waliyofundishwa na kuwataka viongozi wote wa vijana walioaminiwa waajibike kwa nafasi zao, wafanye kazi ili kuhakikisha CCM inakuwa imara zaidi.


"Pia niwaombe vijana kuwa na maadili mema kuheshimu viongozi wa ngazi ya juu na wangazi ya chini, na kuwa na heshima kwa watu wote tusikubali kufanya matendo yasiyokuwa na maadili,kama vile ushoga na usagaji haya matendo hayatakiwi katika jamii na katika Taifa letu, tukemee na kukataa kabisa ili baadae tuweze kuwa na viongozi wenye maadili wanaojielewa"amesema Monalisa.

Katibu wa umoja wa Vijana CCM wilaya Naibu Katalambula wakati akifundisha somo la historia ya CCM amewataka vijana kuheshimu Chama hicho na kufanya kazi kwa kujituma, kama walivyojituma viongozi waanzilishi ambao waliteseka ili kuhakikisha Chama kinasimama imara.

Katibu wa Chama Cha mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Shaban Majeshi amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kukipigania chama ili kuhakikisha 2025 kinachukua tena dolla.

Mjumbe wa baraza jumuia ya vijana Taifa Monalisa Daniel Fausitine akizungumza kwenye semina ya vijana ambapo aliwataka kuyatekeleza yote waliyofundishwa
Mjumbe wa baraza jumuia ya vijana Taifa Monalisa Daniel Fausitine akizungumza kwenye semina ya vijana ambapo aliwataka kuyatekeleza yote waliyofundishwa
Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga Jonathan Madete akizungumza kwenye semina elekezi iliyofanyika Shinyanga mjini
Katibu wa umoja wa Vijana CCM wilaya Naibu Katalambula akizungumza kwenye semina ya vijana wa Uvccm wilaya
Katibu wa umoja wa Vijana CCM wilaya Naibu Katalambula akizungumza kwenye semina ya vijana wa Uvccm wilaya

Katibu wa Chama Cha mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Shaban Majeshi akizungumza na kuwataka vijana kusimama imara wasilegee
Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye semina hiyo ambapo amewaomba vija kuchangamkia fursa ya mikopo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko akizungumza kwenye semina hiyo
Katibu muenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Said Bwanga akizungumza kwenye semina ekekezi ya vijana
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa wa Shinyanga Epafura Masanja akiwaasa vijana
Mwenyekiti mstaafu wa vijana Ccm wilaya ya Shinyanga Dotto Joshua akizungumza kwenye semina hiyo
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuia ya vijana CCM wilaya

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ta Ngokolo akiwasilisha jambo kwa Meya ambapo aliomba wakazi wa Ngokolo wapewe mikopo kwani hawajapewa mkopo toka mwaka 2016

Viongozi wa uvccm wakitoa hoja zao ili wasaidiwe

Viongozi wa uvccm wakitoa hoja zao ili wasaidiwe




Uvccm wakiwa kwenye semina elekezi iliyoandaliwa na viongozi wa Jumuiya hiyo


Wajumbe wa jumuiya hiyo wakiimba na baada ya kuingia viongozi ngazi ya juu

Semina elekezi ikiendelea katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini
Viongozi ngazi ya juu wakiimba baada ya semina hiyo kumalizika




Wajumbe wa jumuiya ya vijana wakiwa kwenye semina hiyo













Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464