Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Sarah Emmanuel akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake
Suzy Luhende, Shinyanga Press
Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shuwasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uendeshaji wa shughuli za kutoa huduma kwa wakazi wa manispaa ya Shinyanga, kutofika kwa mtandao wa majisafi kwa baadhi ya wakazi waliopo pembezoni.
Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Sarah Emmanuel wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo amesema mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Emmanuel amesema changamoto zingine ni kutokuwepo na mfumo wa kuondoa majitaka katika eneo la huduma, uchakavu wa miundombinu unaosababisha kuharibika kwa mabomba na viungio (Fittings) na hivyo kusababisha maji kupotea, ambapo hadi kufikia Juni 2023 kulikuwa na wastani wa upotevu wa maji wa asilimia 21.
"Pia tunakabiliwa na madeni makubwa ya maji yaliyotumiwa na Taasisi na Vikosi vya Ulinzi na Usalama ambavyo mpaka mwezi June 2023 yamefikia kiasi cha Sh 644.7 milioni na ukosefu wa nyenzo za kisasa za kufanyia matengenezo pindi upasukaji wa mabomba makubwa unapotokea,"amesema Mkurugenzi huyo.
Amesema licha ya changamoto hizo pia kuna mafanikio makubwa ambapo
Wananchi zaidi ya 13,000 wa vijiji vya Jomu Buchama na Nyambui kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga
wamenufaika na mradi wa maji ya ziwa Victoria unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na mazingira Shuwasa, ikiwa ni pamoja na wananchi wa kata ya Didia 7,201 wakinufaika na mradi huo.
Emmanuel amesema mamlaka inatekeleza mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba za usambazaji takribani kilomita 8.1 kwa awamu ya kwanza utakaohudumia vijiji vya Jomu na Nyambui ambao umegharimu Sh 24.47 bilioni.
"Sh 24.47 bilioni zilipangwa kutekeleza Mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika miji ya Nzega,Tabora na Igunga, kwa sehemu ya Tinde pekee mradi uligharimu kiasi cha Sh 5.22 na utekelezaji wake ulianza tarehe 21,8,2021 ukiwa umesanifiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 60,000 kutoka katika vijiji 22 ambao tayari umekamilika kwa asilimia 100,"amesema Emmanuel.
Emmanuel amesema kwa sasa Shuwasa inatekeleza ujenzi wa bomba za usambazaji takriban kilomita 8.1 kwa gharama ya Sh 1.1 bilioni na mpaka sasa mamlaka imepokea Sh 905 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 96 na unaendelea kutoa huduma kwa baadhi yamaeneo.
Amesema kiasi cha Sh 333.7 milioni kimetengwa na wizara ya maji kupitia mfuko wa maji kwa ajili ya ujenzi wa mtandao wa majisafi eneo la Didia, na mamlaka tayari imepokea kiasi cha Sh 99.9 milioni kwa ajili ya usambazaji wa bomba weye urefu wa kilomita 8.1 na mradi huo umekamilika kwa asilimia 62 unatarajiwa kukamilika Julai 2023 ambao utanufaisha wananchi 7,201.
Meneja wa kanda ya Tinde kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Joshua Matinde amesema mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 100 ambao utahudumia vijiji vitatu vya Tinde kati ya viji 22 ambavyo ni Jomu, Buchama na Nyambui na mradi huo ni muendelezo wa ujenzi wa mradi wa Tinde Sherui uliotekelezwa na Wizara ya Maji kupitia mkandarasi Megha Engineering and Infrastructure Ltd.
Meneja wa kanda ya Didia kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Innocent Siame amesema tayari mradi wa maji ya ziwa Victoria umekamilika katika kata ya Didia halmashauri ya Shinyanga na baada ya wiki mbili huduma zitaanza kutolewa kwa baadhi ya vijiji vya Didia, ambao una Tangi la kuhifadhia maji lenye ujazo wa mita za ujazo 100.
Mmoja wa wananchi hao Mwanne Deus amesema kabla ya kupata mradi huo walikuwa wakifuata maji zaidi ya kilomita nne, ambapo wanawake na watoto wa kike walikuwa wakitoka alfajiri saa 11 na kurudi saa tano hali ambayo ilikuwa ikisababisha wanawake kupigwa na waume zao na watoto wa kike kubakwa nyakati za usiku wakiwa wanatoka kuchota maji.
"Sisi wananchi wa kijiji cha Didia tuna furaha kubwa sana kupata haya maji tunaishukuru sana serikali, kwani tulikuwa tunapigwa sana na waume zetu pindi tunapochelewa kwenye maji, tulikuwa na ukame mkubwa na shida kubwa katika kijiji hichi sisi hapa tumepata ila tunaomba na vijiji vingine viweze kupatiwa maji,"amesema Deus.
"Kwa kupata maji haya familia zetu zitatulia, ndoa hazitafarakana tena kwa sababu ya maji na watoto wetu hawatabakwa tena kwa sababu tutachota maji karibu, tofauti na pale tulipokuwa tunafuata maji zaidi ya kilomita 4 kwa dumu la lita 20 Sh 500 na wakati mwingine Sh 10000 na tunayapata kwa kupigana ili tuwahi kuondoka"amesema Omary Salumu.
Mery Salumu mkazi wa Kata ya Tinde amesema walikuwa na hamu ya kupata maji muda mrefu lakini kwa sasa wamepata, hivyo wameahidi kuwa wataitunza na watakuwa walinzi ili miundombinu ya maji isiharibiwe na aliwaomba wananchi wengine kuilinda ili iweze kudumu.
Meneja wa kanda ya Tinde kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Joshua Matinde amesema mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 100 ambao utahudumia vijiji vitatu vya Tinde kati ya vijiji 22 ambavyo ni Jomu, Buchama na Nyambui na mradi huo ni muendelezo wa ujenzi wa mradi wa Tinde Sherui uliotekelezwa na Wizara ya Maji kupitia mkandarasi Megha Engineering and Infrastructure Ltd.
Meneja wa kanda ya Didia kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Innocent Siame amesema tayari mradi wa maji ya ziwa victoria umekamilika katika kata ya Didia halmashauri ya Shinyanga na baada ya wiki mbili huduma zitaanza kutolewa kwa baadhi ya vijiji vya Didia,ambao ambao una Tangi la kuhifadhia maji lenye ujazo wa mita za ujazo100.
Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Sarah Emmanuel kushoto Nsianel Gerald afisa mawasiliano katika mamlaka ya maji Shuwasa
Meneja wa kanda ya Didia kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Innocent Siame
Meneja wa kanda ya Didia kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Innocent Siame akionyesha ujazo wa maji
Meneja wa kanda ya Didia kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Innocent Siame akielezea jinsi wananchi walivyofaidika na mradi wa maji ya ziwa Victoria
Mmoja wa wananchi wa Didia akielezea mafanikio ya mradi huo
Mwanne Deus akizungumza na waandishi wa habari na kuishukuru serikali kwa kuwapelekea maji safi na salama
Tangi la kijiji cha Didia
Mmoja wa wananchi wa Didia akielezea mafanikio ya mradi huo
Mmoja wa wananchi wa Didia akielezea mafanikio ya mradi huo
Mmoja wa wananchi wa Didia akikinga maji ya ziwa Victoria
Mmoja wa wananchi wa Didia akikinga maji ya ziwa Victoria
Tangi la maji litakalohudumia vijiji vitatu katika kata ya Tinde