WAZIRI AWESO ATAKA VIJIJI VYA PEMBEZONI MWA ZIWA VICTORIA VIPATE MAJI



wataalamu wa wizara ya maji wameelekezwa kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha vijiji ambavyo vipo pembezoni mwa ziwa  Zictoria vinanufaika na uwepo wa  ziwa hilo ili wananchi wapate suluhisho la kudumu na kupata maji safi na salama.

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri  wa Maji Jumaa Aweso wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nkenge katika halmashauri ya  wilaya ya Misenye ambapo kabla ya mkutano wake wa adhara na wananchi hao alizindua mradi wa maji Katolerwa_Ishozi  ambao unahudumia wananchi wapatao 7278 uliopo kata ya Ishozi.

Waziri Aweso amesema kuwa  mkoa wa Kagera una ziwa Victoria, mto Kagera hivyo maeneo ya vijiji  ambavyo vimeambatana na uanda wa ziwa Victoria  hivyo lazima mpango mkakati uwekwe kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wananufaika na Ziwa.


Amesema kuwa maelekezo hayo yanatakiwa kufanyiwa kazi  na lazima vijiji hivyo vinufaike kwa sababu ni maelekezo pia ya Rais Dkt Samia Suluhu  Hassan  katika dhana yake ya kumtua mama ndoo kichwani.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Nkenge halmashauri ya wilaya ya Misenye Frolent Kyombo amesema kuwa kata ya Ishozi haikuwai kuwa na mradi wa maji huo ni wakwanza ambapo hapo awali wananchi walikuwa wanatumia vyanzo vya maji.

Ameishukuru serikali ya Rais Dkt Samia Suruhu Hassan kwa kuendelea kuwakumbuka wananchi wa wilaya hiyo hasa kwa kutatua changamoto ya maji.

Naye Meneja wa Ruwasa ambao ni wakala wa maji  na usafi wa Mazingira Vijijni Injinia Andrew Kilembe wakati akisoma taarifa ya mradi wa maji Katolerwa_Ishozi amesema kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza Januari 25 2022 na kwa sasa mradi huo umekamilika.

Aidha mradi huo unahudumia wananchi wa vijiji vya Nyarugongo 2543,Katano 1365,Luhano 1708 na Katolerwa 1662 ambapo kwa sasa shughuli zinazoendelea ni kuunganisha maji majumbani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464