Askofu Dkt. Yohana Nzelu
Na Sumai Salum - Kishapu
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Yohana Nzelu amewashauri viongozi wa kanisa,wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa na muda wa kufunga, kuomba na kuwashauri watoto na vijana ambao kwa sasa kumekuwa na wimbi kubwa la uharibifu na utendaji kazi wa shetani ndani yao.
Ameyasema hayoleo jumapili Julai 9 2023 katika Ibada ya sikukuu ya vijana ilioyobebwa na neno "Kijana uwe hodari katika Imani" katika kanisa la KKKT Mhunze usharika wa Hosiana wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Askofu Nzelu amesema kuwa ongezeko la matukio ya ulawiti, ushoga, usagaji na matukio yote ya ukatili ni kwa sababu wanadamu hawataki kuwa chini ya neno la Mungu, watu kutoongozwa na neno la Mungu, kufuata mikumbo ya tamaduni za kigeni zisizofaa sambamba na kutokumheshimu Mungu.
"Nilienda mwaka fulani kwenye utume nchi flani nikakutana na swali kutoka ka mwanamke mmoja akainulizia kuhusu ndoa za jinsia moja nikasema hatutaki kusikia kuhusu suala hilo wala kulijadili akasema ana kijana wake wa miaka 17 na anataka kubadilika kutoka kwenye kijana wa kiume kuwa wa kike, nilipomjibu hivyo nikaonekana mimi wa ajabu sijui kuwapa uhuru na haki watoto na hakuwa tayari kukubaliana na ushauri wangu sasa kanisa tukilegeza msimamo tutatoa hesabu mbinguni siku moja tusikubali ushawishi wowote hata wa kifedha kupindisha neno la Mungu", ameongeza Dkt. Nzelu.
Amewaasa wachungaji kuhubiri neno halisi la Mungu na kuwaasa vijana na watoto kuwa imara kiimani kwani itawasaidia hata nyakati ngumu kutomnung'unikia Mungu akielezea kitabu cha kutoka 15:2 kuwa Musa hakuangalia mazingira bali kutimiza kusudi la Mungu ndani yake na hata nyakati ngumu kama alizopitia Stephano waone mbingu zikifunguka kwa ajili yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Kanisa la KKKT Jimbo la Kusini Mashariki Kishapu na mchungaji kiongozi wa usharika huo wa Hosiana Mch. Patrick Zengo amesema kuwa atahakikisha analifikisha kanisa mahali Mungu amekusudia hasa nyakati hizi za hatari ambapo shetani akilitafuta kanisa kwa hila.
Naye katibu wa vijana kutoka usharika huo Bw. Victory Maganga amesema kuwa kama viongozi wa vijana wanayo mikakati mikubwa ya kuhakikisha vijana wanaishia tabia za kiungu na maadili mema kwa jamii, kanisa na taifa kwa ujumla sambamba na kumtumikia Mungu kwa mali na mioyo yao yote.
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Yohana Nzelu na Mkuu wa Kanisa la KKKT Jimbo la Kusini Mashariki Kishapu na mchungaji kiongozi wa usharika wa Hosiana Mhunze Mch. Patrick Zengo (kulia)
Mkuu wa Kanisa la KKKT Jimbo la Kusini Mashariki Kishapu na mchungaji kiongozi wa usharika huo wa Hosiana Mch. Patrick Zengo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464