CCM yabariki uwekezaji wa bandari, yatoa maagizo serikalini
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Hamashauri Kuu ya chama hicho ambacho kimejadili masuala mbalimbali ikiwemo mkataba wa uwekezaji na uendelezaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai.
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai wakibariki mchakato huo.
Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.
Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.
"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.
Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.
Soma hapa zaidi Chanzo Mwananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464