NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI, AMEAGIZA WANANCHI WA TINDE WASAMBAZIWE HUDUMA YA MAJI
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), kuhakikisha Mkandarasi ambaye anatekeleza kazi ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa vijiji 22 katika Mradi wa Maji Tinde wilayani Shinyanga hadi kufikia mwezi Agosti aanze kazi mara moja.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Amebainisha hayo jana wakati alipotembelea mradi huo katika Tangi la kuhifadhia Maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria, lenye lita za ujazo 1,150,000 lililopo kijiji cha Buchama Kata ya Tinde wilayani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika Mradi wa Maji Tinde.
Amesema mradi huo umeshakamilika kwa asilimia kubwa, na tayari fedha za kusambaza huduma ya maji kwa wananchi zipo, na kuagiza hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu, Mkandarasi huyo aanze kazi ili wananchi wanufaike na mradi huo kwa kupata Majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja,akipanda katika Tangi la Mradi wa Maji Tinde.
“Mkurugenzi wa SHUWASA nakuelekeza wasiliana na Meneja Mradi ili Mkandarasi ambaye anafanya kazi hii ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi hadi kufikia mwezi Agosti awe ameshaanza kazi mara moja na kuvifikia vijiji vyote 22,”amesema Mhandisi Luhemeja.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja,akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa (SHUWASA) CPA Sarah Emmanuel.
Awali, akiwa katika Kata ya Mwalukwa kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji, aliziagiza pia Mamlaka za Maji kutoa elimu kwa wananchi kuvuta mabomba ya maji majumbani mwao, ili kutekeleza adhima ya kumtua ndoo kichwani mwanamke na kuacha kuchota maji kwenye vituo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja,(kulia) akiwa na Mbunge wa Solwa (katikati)Ahmed Salum na Mhandisi wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.
Katika hatua nyingine, amewapongeza wadau wa maendeleo Life Water Intenational, kwa kuiunga mkono Serikali kutekeleza Miradi ya Maji na kutatua changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja,(kulia) akiwa na Mbunge wa Solwa Ahmes Salum, wakimtwisha Ndoo ya Maji Mwanamke mkazi wa Mwalukwa wilayani Shinyanga katika ziara ya kukagua miradi ya maji.
Mradi wa Maji ambao umetekelezwa na Lifer Water.
Naye Diwani wa Tinde Jafari Kanolo, amesema katika mradi huo wa maji Tinde, wananchi waliosambaziwa huduma ya maji ni vijiji viwili tu ambavyo ni Jomu na Nyambai, hata kijiji cha Buchama ambacho Tangi la Maji lilipo nao hawana maji, na kubainisha kuwa huduma ya maji ikipatikana maeneo yote kwenye Kata hiyo itachochea ukuaji wa maendeleo.
Diwani wa Tinde Jafari Kanolo.
Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel, amesema Mkandarasi ambaye amejenga Tangi hilo la Maji ndiyo ambaye atetekeleza kazi ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi, na kuahidi kutekeleza maagizo ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji kwamba Mkandarasi huyo mwezi Agosti ata anza kazi Rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa (SHUWASA) CPA Sarah Emmanuel.
Mbunge wa Jimbo la Solwa wilayani Shinyanga Ahmed Salum, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha na kutekelezwa Miradi ya Maji Safi na salama jimboni mwake, na sasa asilimia kubwa ya wnaanchi hawana changamoto ya huduma hiyo na kubaki vijiji vichache, ambavyo navyo zitatekelezwa miradi ya maji pamoja na taasisi zote za Serikali.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum.
Nao baadhi ya wananchi ambao wamepata huduma ya Majisafi na salama ya Ziwa Victoria, wameishukuru Serikali kwa kuwatekelezea miradi hiyo ambayo imewaondolea changamoto ya kutafuta maji umbali mrefu na kupoteza muda wa kufanya shughuli za maendeleo, huku wengine ndoa zao zikiingia matatani kwa kudhaniwa wamekwenda kuchepuka kumbe wamefuata maji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja wapili (kushoto) akiwa na Mbunge wa Solwa Ahmed Salum, na (kulia) ni Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela, pamoja na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emmael Nkopi, katika ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Shinyanga.
Ziara ikiendelea ya ukaguzi wa miradi ya maji.
Tangi la Mradi wa Maji Ishinabulandi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akiwa na Mbunge wa Solwa Ahmed Salum (katikati) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje wakiangalia mradi wa maji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, akiwa katika shule ya Bulambila wilayani Shinyanga akiangalia mradi wa Majisafi na salama shuleni hapo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika Mradi wa Maji Tinde.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, akiimba wimbo wa Tanzania na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bulambila wilayani Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464