Wanaume wadai kurukishwa kichurachura kupewa tendo la ndoa.

Meneja Mradi wa Haki ya Afya kwa Maendeleo ya Binti kutoka Shirika la Smile For Community, Aneth Kiyao aliongea katika kikao cha viongozi wa vijiji na mitaa katika Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Baadhi ya wanaume wa Halmshauri ya mji Nanyamba mkoani Mtwara wamelalamika kunyanyaswa na wake zao wakati wakitaka unyumba kwa kupewa masharti ikiwemo kurukishwa kichurachura kuzunguka kitanda.
Akizungumza leo Julai 11 katika warsha ya viongozi wa serikali za vijiji katika halmshauri hiyo iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Smile for Community linalofadhiliwa na Legal Services Facility, Mwenyekiti wa Mtaa wa Namkuku, Andrew Mathew amesema tabia hiyo imechukuliwa ni unyanyasaji wa kingono.
Soma hapa zaidi Chanzo Mwananchi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464