BENKI KUU WAMEFANYA MKUTANO NA WADAU MKOA WA SHINYANGA

BENKI KUU WAFANYA MKUTANO NA WADAU MKOA WA SHINYANGA.

Na. Shinyanga RS.

Benki Kuu Tawi la Mwanza wamefanya mkutano na wadau wake kwa lengo la kukumbushana namna bora ya kushirikiana katika upatikanaji wa taarifa mbalimbali za TRA, kilimo, mifugo, madini, tumbaku, mamlaka ya uhifadhi wa chakula Tanzania, mazao ya nyuki nk ili ziweze kusaidia uandaaji wa mipango ya kiuchumi.

Akizungumza wakati wa mkutano huu Dkt. Deogratias Philip Macha ambaye ni Meneja Idara ya Uchumi kutoka Benki Kuu Tawi la Mwanza alisema kuwa ili kufanikisha vema utekelezaji wa majukumu ya Benki Kuu inahitaji sana ushirikiano kutoka kwa Idara na Taasisi mbalimbali na ndiyo sababu ya Benki Kuu ukufanya mkutano huu na wadau utakaokuwa na lengo la kuwakumbusha ili kuweza kushirikiana katika upatikanaji huu muhimu wa taarifa.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kufanya mkutano huu muhimu na wadau wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kukumbushana namna bora ya ushirikishwaji na utoaji wa taarifa za kiuchumi kutoka kwa Idara na Taasisi mbalimbali hapa Mkoa wa Shinyanga na Halmashauri zake zote hasa katika eneo la TRA, kilimo, madini, tumbaku, Mamlaka ya Uhifadhi wa Chakula Tanzania, mazao ya nyuki nk ambapo pia kupitia mkutano huu tutapata tathimini ya utekelezaji wa maadhimio yaliyowekwa mwaka uliopita ili kuona kama yalifanikiwa na kwa kiwango kipi," akisema Dkt. Macha.

Awali akifungua mkutano huu muwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dafroza Ndalichako ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa, Mkoa wa Shinyanga unashirikiana na Benki Kuu Tawi la Mwanza katika kuhakikisha taarifa hizi muhimu za kiuchumi zinapatikana.

Sambamba na taarifa nyingine kutoka katika Idara zilizotajwa ilimkuweza kuandaa taarifa ya kuelezeaTaifa, hivyo akawakaribisha sana Benki Kuu huku akiwataka washiriki kufuatilia kwa umakini mada zilizoletwa na wataalamu hao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464