Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amefanya ziara mkoani Shinyanga kukagua utoaji wa huduma bora za Afya za matibabu, pamoja na kukabidhi vifaa tiba vya wodi ya watoto wachanga mahututi.
Waziri wa Ummy Mwalimu (kushoto) akikabidhi Vifaa Tiba kwa ajili ya watoto wodi za watoto wachanga mahututi, kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Amefanya ziara hiyo leo Julai 13,2023 kwa kuzungumza na watumishi wa huduma za Afya, Wagonjwa, pamoja na kutembelea kuona namna huduma za Afya zinavyotolewa kwa Wananchi katika Hospitali ya Manispaa na Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akikabidhi vifaa tiba.
Amesema amefarijika kuona huduma za Afya zinatolewa vizuri kwa wagonjwa, na kusema kwamba Rais Samia ataendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma bora za Afya, pamoja na kuokoa Afya za watoto wachanga na Njiti.
Muonekano wa vifaa tiba.
"Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 6.3 kwa ajili ya kununua vifaa tiba nchi nzima, kwa ajili ya watoto Wachanga na Njiti kuokoa Afya zao, na leo hapa mkoani Shinyanga nakabidhi Vifaa hivi vyenye thamani ya Sh.milioni 170 katika Wodi ya Watoto Mahututi,"amesema Waziri Mwalimu.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisalimiana na wagonjwa hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.
"Vifaa hivi vitapelekwa pia katika Hospitali ya Kahama na Kishapu, Rais Samia anataka kila Mama Mjamzito aondoke na kichanga chake kikiwa salama haijarishi kimezaliwa na uzito kiasi gani, ndiyo maana akatoa vifaa tiba,"ameongeza.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiangalia vifaa tiba CT-SCAN.
Aidha, amewataka pia Madaktari pamoja na wauguzi kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa, pamoja na kutumia lugha nzuri.
Katika hatua nyingine, amewataka Madaktari na watoa huduma za Afya wakiwamo wauguzi, kuzingatia miiko na maadili ya taaluma zao na kuacha tabia ya kutoa siri za wagonjwa.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Amesema si maadili ya kitaaluma daktari au mtoa Huduma ya Afya kutoa siri za Mgonjwa, na kubainisha kuwa watakao endelea kukiuka miiko ya utoaji huduma za Afya na kuwafikisha Pabaya watasimamishiwa Lesseni zao.
"Hapa naangalia kwenye Mitandao ya Kijamii naona kuna taarifa ya Mwanume kuwa amejikata uume kwamba hataweza kufanya mapenzi tena, nimemuagiza Mganga Mkuu alifuatilie hilo nani katoa taarifa ya Mgonjwa,"amesema Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Pia amewataka Wafamansia wafanye maoteo sahihi ya dawa, ili upatikanaji wa dawa uwepo kwa wananchi, na siyo kuwepo na dawa kwenye Makaratasi lakini uhalisia hakuna dawa.
Amewaagiza pia Wakurugenzi wa Halmashauri, kuajiri Wataalamu wa Afya wa Mkataba kupitia fedha za mapato ya ndani, ili kupunguza tatizo la upungufu wa tumishi katika Sekta ya Afya,wakati Serikali ikiendelea kutatua tatizo hilo.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Yudas Ndungile, akisoma taarifa ya huduma za Afya mkoani humo, amesema upatikanaji wa huduma umeimarishwa pamoja na upatikaji wa dawa asilimia 89.9.
Amesema licha ya huduma hizo kuboreshwa, lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ya upungufu wa watumishi na Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufani mkoani humo, pamoja na Magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) na hakuna Jengo la kuhifadhia maiti Mochwari.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, alimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kuboresha huduma za Afya mkoani humo, na kuahidi maelekezo ambayo ameyatoa Waziri watayatekeleza.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza na Watumishi wa Afya Mkoani Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. Luzila John akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na kutoa taarifa ya Hospitali hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Wataalamu wa Afya wakiwa kwenye ziara ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Watumishi wa Afya wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Awali Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kushoto) akiwasilia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Luzila John (kulia)akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kumaliza kuzungumza na kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464