WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU APIGA MARUFUKU WANANCHI KUUZIWA DAWA ZA MALARIA


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu apiga marufuku wananchi kuuziwa dawa za Malaria

Na Marco Maduhu, KISHAPU

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amehitimisha ziara yake mkoani Shinyanga, kwa kutembelea huduma za Afya wilayani Kishapu, kukagua utoaji wa huduma bora za matibabu, huku akipiga Marufuku wananchi kuuziwa dawa za Malaria katika huduma za Afya.

Amebainisha hayo leo Julai 14,2023 wakati akizungumza na Wananchi alipotembelea kituo cha Afya Negezi wilayani Kishapu, na katika ziara hiyo ametembelea hospitali ya wilaya, kituo cha Afya Negezi na Zahanati ya Maganzo, pamoja na kuongea na watumishi wa Afya.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Akizungumza na wananchi wa Negezi, amesema ni marufuku Mwananchi kulipia kipimo cha Malaria kile cha kudungwa kidole, dawa ya Alu, SP, na Sindano ya Malaria kali, isipokuwa kipimo cha BS ndicho wanapaswa kulipia.

"Mwananchi ukitozwa hela yoyote nipigie simu, hakuna kutoa pesa matibabu ya Malaria ni bure, isipokuwa kipimo cha BS," amesema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kumuombea Afya njema Rais Samia, ili aendelee kuwaletea maendeleo watanzania ikiwamo kuboresha huduma za Afya na kupata matibabu bora.

Amesema Serikali kupitia Wizara hiyo ya Afya,itaendelea kutatua changamoto moja baada ya nyingine katika huduma za Afya, likiwamo la upungufu wa watumishi, Magari ya Wagonjwa pamoja na kuongeza Majengo yakiwamo ya huduma ya Mama na Mtoto.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, akiteta Jambo na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.

"Katika wilaya hii ya Kishapu tutaendelea kuboresha huduma za Afya, pamoja na kutoa Magari Matatu ya Wagonjwa, mawili yatatolewa na TAMISEM na Moja kwenye Wizara yangu," amesema Waziri Ummy.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi wilayani humo na kuboresha utolewaji wa huduma za Afya ikiwamo na kujengwa vituo vya Afya na Zahanati.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo.

Awali, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akitoa taarifa ya huduma ya Afya wilayani humo, ameishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za matibabu wilayani humo, na kubainisha baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili likiwamo tatizo la upungufu wa watumishi wa Afya 874.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.

Amesema wilaya hiyo ina hospitali mbili, Moja Serikali na nyingine ya Binafsi, Vituo vya Afya 64, na Zahanati 51, na pia inakabiliwa na upungufu wa Magari ya kubebea Wagonjwa, ambapo Waziri aliahidi kuwapatia Magari Matatu, Mawili kutoka TAMISEM na Moja Wizara ya Afya.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika Stoo ya dawa kituo cha Afya Negezi wilayani Kishapu.

Nao baadhi wa Wananchi wilayani Kishapu akiwamo Ester Lugangeka, wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa huduma hizo za Afya kuwa karibu na makazi yao zikiwamo huduma za upasuaji na kuokoa Afya zao.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amehitisha ziara yake ya siku mbili leo Mkoani Shinyanga iliyokuwa na lengo la kukagua utoaji wahuduma bora za matibabu, pamoja na kubaini changamoto ambazo bado zinaikabili Sekta ya Afya na kuzitafutia ufumbuzi.
Wananchi wa Negezi wilayani Kishapu wakimsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Wananchi wa Negezi wilayani Kishapu wakiendelea kumsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Wananchi wa Negezi wilayani Kishapu wakiendelea kumsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Wananchi wa Negezi wilayani Kishapu wakiendelea kumsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Wananchi wa Negezi wilayani Kishapu wakiendelea kumsikiliza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ziara hiyo ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Kishapu Jakaya Kikwete, (kushoto)ni Bunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo na (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiendelea na ziara yake katika Hospitali ya wilaya ya Kishapu Jakaya Kikwete.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo alipowasili wilayani Kishapu kufanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma za Afya.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Emmanuel Johnson alipowasili wilayani Kishapu kufanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma za Afya.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Kishapu Benard Werema alipowasili wilayani Kishapu kufanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma za Afya.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464