Wakuu wa mikoa, wilaya watajwa ripoti ya haki jinai
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya tume hiyo kwenye hafla iliyofanyika leo Julai 15, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema kuwa wakuu wa mikoa, wilaya ni kosa kisheria kujitambulisha kama wenyeviti wa kamati ya Ulinzi na Usalama.
Tume ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai nchini imebaini kuwa wakuu wa mikoa na wilaya hujitambulisha kama wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama kinyume na sheria inayowatambua kama wenyeviti wa kamati za usalama.
Pia, Tume hiyo imebaini kuwa wakuu hao huambatana na kamati za usalama katika ziara zao hali inayosababisha hofu kwa wananchi na kuwafanya washindwe kufikisha kero zao kwa kuogopa kukamatwa, kuongeza gharama kwa Serikali kutokana na matumizi ya magari na posho wanazolipwa watumishi hao kwenye ziara hizo.
Akisoma taarifa rasmi ya Tume leo Jumamosi Julai 15, 2023 Ikulu Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema Tume imependekeza wakuu wa mikoa na wilaya wasijitambulishe kama wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama.
Soma hapa zaidi chanzo Mwananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464