Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU UMEZINDUA MRADI WA MAJI BUGAYAMBELELE ULIOTEKELEZWA NA SHUWASA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, (kushoto) akimtwisha ndoo ya maji Mwanamke Fotunata Malongo Mkazi wa Bugayambelele akiwa na Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.

MWENGE WA UHURU UMEZINDUA MRADI WA MAJI BUGAYAMBELELE ULIOTEKELEZWA NA SHUWASA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MWENGE wa Uhuru umezindua mradi wa maji wa Bugayambelele uliopo Manispaa ya Shinyanga, ambao umetekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA.

Mradi huo umezinduliwa leo Julai 28, 2023 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim.
Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel akitoa taarifa ya mradi.

Akizungumza wakati wa kutoa Taarifa za utekelezaji wa Mradi huo wa Maji Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA CPA Sarah Emmanuel, amesema mradi huo wa Majisafi na salama kutoka Mtandao wa Ziwa Victoria utanufaisha wananchi wapatao 10,165.

“Mradi huu wa Maji gharama zake ni Milioni 279.4 ambapo wananchi wataondokana na adha ya kutafuta maji umbali mrefu,” amesema CPA Emmanuel.
Kiogozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, akifungua Maji kabla ya kuuzindua mradi huo.

Naye Kiogozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, ameipongeza SHUWASA kwa kutekeleza mradi wa maji kwa kiwango bora na thamani ya fedha imeonekana, sababu wamepitia nyaraka zote za utekelezaji wa mradi huo na kujiridhisha umejengwa kwa ufasaha,
Kiogozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, akizinda mradi wa maji.

“Tunampongeza pia Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo hii ya Maji na kumtua ndoo kichwani mwanamke,”amesema Kaim.

Nao baadhi ya wananchi wa Bugayambelele, ameishukuru Serikali kwa kuwatekelezea Mradi huo wa Maji, ambao umewaondolea adha ya kufuata maji umbali mrefu.

Post a Comment

0 Comments