Paroko auawa Karatu
Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Karatu mkoani Arusha, Pamphili Nada, ameuwa kwa kupigwa na kitu kizito na mtu anayesadikiwa kuwa na matatizo ya afya akili ambaye alilazimisha kuingia kanisani kwa madai ya kutaka kusali.
Hata hivyo baada ya mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30) kufanya mauaji hayo, nae akauawa na wananchi wenye hasira.
Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha leo Jumatano Julai 19, 2023 kutokea mauaji hayo.
Soma hapa zaidi chanzo Mwananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464