TAASISI ZA ELIMU YA JUU KUENDELEA KUSHIRIKINA NA JESHI LA POLISI KUKABILIANA NA UHALIFU NCHINI


TAASISI ZA ELIMU YA JUU KUENDELEA KUSHIRIKINA NA JESHI LA POLISI KUKABILIANA NA UHALIFU NCHINI.

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi-Dar es salaam.

Taasisi za elimu ya juu ndani na nje ya nchi, zimeendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini katika kukabiliana na uhalifu ambapo, Taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) imekuwa na taratibu za kushirikiana na taasisi mbalimbali hapa Nchini kutoa mafunzo na mchango wa moja kwa moja kwa Taasisi za umma na binafsi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru Dk. Bakari George wakati wa kuwasilisha mada mbalimbali katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa wakati chuo hicho kinatimiza miaka siti (60) katika kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.

Dk. George ameongeza kuwa bado kuna matukio ya ukatili wa kijinsia katika baadhi ya maeneo hapa Nchini ambapo amesema kwa ushirikiano huu ambao umeanza baina ya Jeshi la Polisi na Taasisi hiyo utakwenda kukomesha vitendo vya ukatili katika jamii ya watanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dk. Lazaro Mambosasa amesema kuwa chuo hicho kimejipanga kupokea mafunzo hayo kwa kundi la wakufunzi na wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi huku akibainisha kuwa wahalifu wao wanashirikiana katika uhalifu ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo litaendelea kushirikiana na taasisi za elimu kukomesha vitendo vya ukatili.

Nae Mkufunzi Mkuu (CI) kamishna msaidizi wa Polisi ACP Andrew Legembo amesema kwa kupata mafunzo hayo kutaongeza maarifa na silaha katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na watoto hapa nchini ambapo amekishukuru chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru kwa kuwa kinara wa kufundisha masuala ya ukatili wa kijinsia.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464