AFISA MASOKO KOLANDOTO JOSEPHINE CHARLES AMESHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA SHULE YA OLA BUGISI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
AFISA Masoko Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga Josephine Charles, amesherehekea siku yake ya kuzaliwa katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Awali na Msingi (OLa English Medium Pre and Primary School) iliyopo Bugisi Kata ya Didia wilayani Shinyanga.
Wanafunzi na Walimu wakimuimbia wimbo katika siku yake ya kuzaliwa Josephine Charles wa 'Happy Birthday'
Sherehe hiyo imefanyika leo Julai 23,2023 katika shule ya Ola, na kutoa vifaa mbalimbali vya shule kwa ajili ya kuiunga Mkono Serikali kuboresha mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma na kufanya vizuri kitaaluma.
Josephine Charles akikabidhi Madaftari kwa Walimu.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo, amesema kila mwaka anapokuwa akisherehekea kumbukizi yake ya kuzaliwa, amekuwa akifanya shughuli mbalimbali za kijamii, pamoja na kutoa zawadi wakiwamo akina mama ambao hujifungua katika huduma za Afya ikiwamo Hospitali ya Kolandoto.
Josephine Charles akizungumza.
"Ni desturi yangu kila ninaposherehekea siku yangu ya kuzaliwa kufanya shughuli za kijamii,na leo nimeamua kuinga mkono Serikali kuboresha taaluma na kutoa vifaa vya shule, ili wanafunzi wasome katika mazingira rafiki na kutimiza ndoto zao," amesema Josephine.
Aidha, ametaja vifaa vya shule ambavyo ametoa ni Daftari na Kalamu, huku pia akitoa Mchele,Juice,Pipi, chumvi pamoja na Sabuni.
Muonekano wa zawadi alizotoa.
Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa wanafunzi wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao ambapo baadae watakuja kuwa viongozi wa Taifa hili.
Josephine Charles akizungumza na wanafunzi.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Sister Comfort Amevor, amemshukuru mzazi huyo kwa kuunga mkono elimu, na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na wanafunzi na kutoa zawadi ya vifaa vya shule.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Ola Sister Comfort Amevor,
Amesema, shule hiyo imekuwa pia ikisaidia kusomesha watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu, na imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma na wanafunzi kupata matokeo mazuri.
Mhasibu wa Shule hiyo Sister Mary Mtui akizungumza kwenye Sherehe hiyo ya siku ya kuzaliwa Josephine Charles.
Josephine Charles akikabidhi zawadi kwa Walimu.
Josephine Charles akikabidhi zawadi ya Kalamu kwa Walimu.
Josephine Charles akikabidhi zawadi ya Mchele kwa Walimu.
Wanafunzi na Walimu wakimuimbia Josephine Charles wimbo wa katika siku yake ya kuzaliwa wa 'Happy Birthday'
Josephine Charles akifurahia jambo na wanafunzi.
Josephine Charles akipiga picha ya pamoja na Walimu ambao ni Ma-Sister katika shule ya OLA.
Josephine Charles akipiga picha ya pamoja na Walimu ambao ni Ma-Sister katika shule ya OLA.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa katika Sherehe ya siku yake ya kuzaliwa Afisa Masoko Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga Josephine Charles.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464