WANANCHI WATUMIA MAJI MACHAFU,MKANDARASI AKIDAIWA KUUTELEKEZA MRADI WA MAJI
Na Marco Maduhu, KAHAMA
WANANCHI wa kijiji cha Mwaningi Kata ya Bulige Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, wamelalamika kuendelea kutumia maji machafu ya kwenye Mabwawa na kuhatarisha Afya, huku Makandarasi ambaye anatekeleza mradi wa Maji kijijini humo amedaiwa kuutekeleza.
Maji ambayo wanatumia wananchi kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani.
Wamebainisha hayo jana kwenye ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi.
Mmoja wa wananchi hao Malita Charles, amesema kijiji hicho kina kabiliwa na uhaba mkubwa wa Majisafi na Salama, na wamekuwa wakitumia maji ya kwenye mabwawa kwa matumizi yote ya nyumbani ikiwamo na kunywa, na kuiomba Serikali iwakamilishie mradi huo wa maji kijijini humo, ili wasitumie tena maji machafu.
Mwanachi Malita Charles.
“Hapa kijijini hatuna maji salama tunatumia maji machafu ya kwenye mabwawa likiwamo bwawa lilepale, na maji ya kunywa hua tunaweka dawa ya kusafisha maji (shabu) angalau yavutie hata kuyanywa tuna shida kweli ya maji,”amesema Malita.
Mwananchi mwingine Modesta Masai, amesema matumizi ya maji hayo machafu yamekuwa yaki hatarisha Afya zao na hata kupata magonjwa ya matumbo ya mara kwa mara.
Mwananchi Modesta Masai akitoka kuchota maji ya kwenye bwawa.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameagiza Mkandarasi ambaye ametekeleza mradi wa maji kutoka Kampuni ya Pet Cooperation Limited kwamba hadi kufikia kesho (Jumatatu), awe amesha Ripoti kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama, pamoja na kurudisha pesa za Serikali ambazo alikwisha chukua kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja.
“Muongozo wa Wizara unasema Makampuni ambayo yanashindwa kufanya kazi yafutwe kabisa nah ii kampuni ni moja wapo liwekwe kwenye (Black List) sababu lengo kuu la Serikali kutumia Wakandarasi kutekeleza haraka miradi hii ya maji ikamilike haraka, lakini huyo ameleta dharau,”amesema Mhandisi Luhemeja.
Mradi wa maji ambao umetelekezwa na Mkandarasi.
Aidha, amemuagiza Meneja Wakala wa Maji Safi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela, kwamba pesa ambazo atazirudisha Mkandarasi huyo wapewe wananchi wa kijijini humo na kuanza kuchimba Mitaro ya Mabomba, na Mradi huo utekelezwe kwa Force Account na ukamilike Oktoba mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, (kulia) akiwa na Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.
Kwa upande wake Meneja huyo wa Ruwasa, amesema Mradi huo wa Maji ulianza kutekelezwa mwaka jana mwezi Februari na ulikuwa ukamilike June mwaka huu kwa gharama ya Sh.bilioni 2.2, lakini Mkandarasi ameutelekeza huku akiwa ameshachukua baadhi ya fedha, na wakimtafuta wakae wazungumza hapatikani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, (kushoto) akiwa na Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.
Tangi la Maji katika kijiji cha Mwatobo Halmashauri ya Msalala.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika Tangi la Maji Bugarama katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi,
Tangi la Mradi wa Maji Bugarama.
Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maji ikiendelea.
Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maji ikiendelea.
Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maji ikiendelea.
Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maji ikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464