WANANCHI WAMUOMBA RAIS SAMIA AWARUHUSU WAENDELEE KUISHI NDANI YA HIFADHI MSITU WA NINDO WILAYANI SHINYANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WANANCHI wa vijiji Sita wilayani Shinyanga ambao wamevamia eneo la Hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani humo, wamemuomba Rais Samia, awaache waendelee kuishi kwenye hifadhi hiyo, kutokana na eneo ambalo wamemegewa kuishi ndani ya hifadhi wamedai ni finyu sababu kuna watu tayari wanaishi.
Hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani Shinyanga, ilitambuliwa kisheria na kutangazwa na gazeti la Serikali Namba 10 mwaka 1958, ikiwa na ukubwa wa Hekta 27,446, lakini baada ya wananchi kuvamia na kuishi humo, eneo la hifadhi limesalia hekta 10,969, ambapo Serikali ikaona Hekta 3,726 iwamegee wananchi ili waishi, na Hekta 7,243 zibaki kwa ajili ya hifadhi.
Wamebainisha hayo jana kwenye Mkutano wao wa hadhara ambao ulikuwa na ajenga moja tu ya kumuomba Rais Samia awaache waendelee kuishi ndani ya hifadhi hiyo.
Mmoja wa wananchi hapo Peter Buhemba, amesema wanamshukuru Rais Samia kwa kuwa jali na kuwatengea eneo la Makazi ndani ya hifadhi hiyo, lakini eneo hilo haliwatoshi sababu kuna watu tayari wanaishi na wanamiliki mashamba, na kuhofia kuna weza tokea Migogoro ya ardhi na hata kukosa maeneo ya kufanya shughuli za kilimo.
Mwananchi mwingine Silvester Shimbolya, amesema eneo hilo ambalo wametengewe lingekuwa halina wananchi ambao wanaishi linge watosha na kuishi kwa Amani, sababu wangefanya shughuli zao za kilimo na ufugaji bila ya bughuza yoyote, lakini sasa hivi wanahofia usalama wao sababu watakwenda kuishi katika maeneo ambayo yana watu wengine.
“Sisi hatujagoma kuondoka hifadhini isije kutafsiliwa vingine, ila tunaombi tu kwa Rais na Serikali yake sikivu, atuache tuendelee kuishi humu hifadhini, hifadhi hii ibaki tu kuwa eneo la makazi sababu tumeishi humu miaka na miaka na sasa tumezeeka, huko tunapopelekwa eneo ni finyu tutaingia kwenye mafarakano na wenzetu ambao tayari wanaishi eneo hilo,” amesema Shimbolya.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Lyamidati Dotto Mende, amesema wananchi wa vijiji hivyo sita wapo zaidi ya 1,000 na baadhi ya Kaya moja ina watu kuanzia 10 hadi 30, na hofu yao kubwa ni kukosa maeneo ya kulima mashamba, sababu maisha yao yanategemea kilimo na eneo ambalo wametegewa kuishi ni finyu lakini kusingekuwapo na watu lingewatosha.
Aidha, hivi karibuni Mhifadhi Mkuu Daraja wa Pili kutoka Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS)Kanda ya Magharibi Lucas Nyambala, akiwa mkoani Shinyanga katika kikao cha kujadili utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri Nane Kisekta juu ya utatuzi wa Mgogoro wa hifadhi hiyo, amesema Serikali ili ridhia wananchi wasiondolewe eneo lote la hifadhi bali watengewe eneo la kuishi hekta hizo 3,726 na hekta 7,243 zibaki kwa ajili ya hifadhi.
Vijiji Sita ambavyo vimevamia eneo la Hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani Shinyanga, ambavyo vinapaswa kupisha maeneo ya hifadhi na kwenda kuishi katika eneo ambalo wametengewa na Serikali ndani ya hifadhi hiyo ni Ng’homango, Mwabundala, Lyamidati, Kadoto, Mwajiji na Buzinza.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lyamidati wilayani Shinyanga Dotto Mende akifungua Mkutano kwa niaba ya Wenyeviti wenzake kutoka vijiji Sita, wa kumuomba Rais Samia awaruhusu waendelee kuishi ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani humo.
Wananchi wakiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo wa kumuomba Rais Samia awaruhusu waendelee kuishi ndani ya hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani Shinyanga.
Mwananchi Wille Nyanda akizungumza kwenye Mkutano huo wa kumuomba Rais Samia awaruhusu waendelee kuishi ndani ya hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani Shinyanga.
Wananchi wakiendelea kuzungumza.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa kumuomba Rais Samia awaruhusu waendelee kuishi kwenye Hifadhi ya Msitu wa Nindo wilayani Shinyanga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464