VIJANA WATATU MBARONI TUHUMA KUBAKA MWANAFUNZI AKITOKA DUKANI


WATATU MBARONI TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI KAHAMA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi

Na Halima Khoya,Shinyanga.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia vijana watatu wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kumbaka Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kishimba (Jina lake limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 14 akitoka dukani kwenda nyumbani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP Janeth Magomi amesema tukio la ubakaji limetokea Julai 08 2023 majira ya saa 07 mchana Kijiji cha Igumhwa Kata ya Kitwana Halmashauri ya Wilaya Kahama Mkoani humo.


Magomi amesema kuwa vijana waliokamatwa ni Dotto Venancy (18),Juma Mwita (17) na Paul Peter (17) ambao walihusika kumshambulia binti huyo aliyekuwa akitoka dukani kwenda nyumbani ambapo alibakwa na kijana aliyemfahamu kwa sura.



Amesema chanzo cha tukio hilo ni mmomonyoko wa maadili ambapo mmoja wa watuhumiwa hao ametoroka baada ya kutenda kosa hilo.


"Wito kwa jamii, wazazi na Walezi wanatakiwa wawe karibu watoto kwa kuwalea katika maadili ya kidini,kwasababu kumekua na changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii",amesema Magomi.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464