WATOTO WANUSURIKA KIFO NYUMBA IKITEKETEA MOTO KAHAMA

Na Kareny Masasy, Kahama 

MTOTO wa miaka tisa imedaiwa kumuokoa mtoto mwenzake wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa ndani baada ya nyumba yao kuanza kuteketea kwa Moto mtaa wa Mhongolo manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga. 

Imedaiwa nyumba hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Mjane Asha Maziku ambapo alieleza kuwaacha wijukuu zake nyumbani huku akienda kwenye shughuli zingine za kifamilia.

 Akiongea na mwandishi wa habari nyumbani kwake Maziku amesema anafikiri chanzo cha Moto huo ni shoti ya Umeme sababu alielezwa na mashuhuda kuwa Moto ulianzia kuwaka juu ya nyumba na awali shoti ya Umeme ilikwisha wahi tokea kwenye nyumba hiyo. 

"Nina ishi na wijukuu zangu wanne wawili wanasoma ambapo ndani kulikuwa na watoto hao wadogo Moto ulivyoanza walibebana kutoka nje hakuna aliyefariki bali Mali zangu zote zimeteketea ndani"amesema. Maziku.

Amesema kuna watu amesikia walisema ni jiko la gesi limesababisha lakini siyo kweli kwani mtungi wa gesi uliisha ni kipindi cha miezi sita Sasa. Shakra Mohamed ambaye ni mdogo wake na Asha pia ni jirani alisema Moto huo waliona kuanza kuwaka juu ya nyumba majira ya saa moja na dakika Arobaini na tano na walipiga simu ofisi za zimamoto na uokoaji lakini walichelewa kutoka hadi majira ya saa tatu usiku. 

Mwenyekiti wa mtaa wa Mhongolo Emanuel Nangale alisema chanzo cha Moto hakifahamiki lakini alitoa ushauri kwa wananchi kutowaacha watoto wadogo peke yao ndani ya nyumba watoto wamejiokoa wenyewe hiyo ni hatari. "Kweli wananchi wameponda mawe gari la zimamoto na uokoaji lilikuwa likitokea ofisi za Buzwagi wakifikiri limetoka manispaa baada ya kuona limechelewa kufika kwa wakati Ila polisi waliofika nakuzuia" amesema Nangale . 

Mkaguzi zimamoto na uokoaji wilaya ya Kahama Edward Selemani alisema wananchi walipiga simu nakuelezwa gari ni bovu lakini wao wakafanya jitihada za kuazima gari kutoka Buzwagi lilipofika wananchi wakaanza kuponda mawe ndipo wakaomba ulinzi wa jeshi la polisi ili kuweza kuuzima usiweze kusambaa kwenye nyumba za jirani.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464