MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KISHAPU,WANANCHI WAHIMIZWA KUTUNZA MAZINGIRA,VYANZO VYA MAJI

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KISHAPU,WANANCHI WAHIMIZWA KUTUNZA MAZINGIRA,VYANZO VYA MAJI

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MWENGE wa uhuru umezindua na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kishapu, huku wananchi wakihimizwa kutunza Mazingira pamoja na vyanzo vya maji.

Kauli mbiu ya mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu (2023) inasema' Tunza Mazingira,Okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe Hai kwa uchumi wa Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia)akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Kishapu Josephe Mkude kwa ajili ya kuukimbiza wilayani humo na kuipitia Miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzinduliwa, mara baada ya kumaliza kuupokea kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk,Yahaya Nawanda.

Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Shinyanga, umeanza kukimbizwa leo wilayani Kishapu kwa umbali wa kilomita 118 pamoja na kuifikia Miradi Sita yenye thamani ya Sh.bilioni 1.3.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, amesema ameridhika na miradi hiyo ya maendeleo wilayani Kishapu, na yote ameizindua hakuna hata mmoja ambao umekataliwa, huku akiwataka wananchi watunze mazingira na vyanzo vya maji.

"Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo, na leo nimeikagua na kuizindua tumpongeze sana Rais wetu,"amesema Karim.

Aidha, akiwa katika upanuzi wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria wa Maganzo- Masagala, amesema mradi huo ni muhimu sana katika kutatua Changamoto ya wananchi kufuata maji safi na salama umbali mrefu pamoja na kumtua ndoo kichwani Mwanamke.

Naye Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi jimboni humo na kutekelezwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwamo hiyo ya Maji.

Miradi ya maendeleo ambayo imepitiwa na Mwenge wa Uhuru kuwa ni Barabara ya Buganika- Kabila Kilomita 11, vyumba viwili vya Madarasa na vyoo Sita katika shule ya Msingi ya Awali Idukilo.

Miradi mingine ni Kituo cha Afya Negezi, Mradi wa Maji Maganzo- Masagala, Mradi wa kuhifadhi Mazingira na vyanzo vya Maji katika Bwawa la Songwa, Klabu ya wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Maganzo na kuweka jiwe la Msingi Stendi ya Maganzo.

Mwenge huo Uhuru Kesho utakimbizwa Katika Manispaa ya Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim akizindua Mradi wa Barabara ya Buganika-Kabila.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim, akizundua vyumba viwili vya Madarasa na Matundu Sita ya Choo katika Shule ya Awali Idukilo.
Vyumba viwili vya Madarasa shule ya Awali Idukilo.
Kituo cha Afya Negezi kikizinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim akizindua Mradi wa Maji wa Maganzo- Masagala.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim, akimtwisha ndoo ya Maji Mwanamke Ester Gonji mara baada ya kumaliza kuzindua mradi wa maji wa Maganzo- Masagala.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim akizindua mradi wa utunzaji Mazingira na Vyanzo vya Maji katika Bwawa la Songwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim akipanda mti katika mradi wa utunzaji mazingira na vyanzo vya maji katika Bwawa la Songwa
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akipanda Mti.
Wanafunzi wakipanda Miti.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim, akizindua Klabu ya wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Maganzo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim,(kulia)akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu.
Viongozi wilayani Kishapu wakiwa kwenye Mbio za mwenge wa Uhuru.
Viongozi wilayani Kishapu wakiwa kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim (katikati) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) na Mbunge wa Kishapu (Kulia) Boniphace Butondo.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilayani Kishapu Benard Werema akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Meneja RUWASA wilayani Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima akiwa wameushika Mwenge wa Uhuru.
Diwani wa Maganzo Mbaru Kidiga akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464