MWENGE WA UHURU WAZINDUA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA TAWI LA SHINYANGA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim (kulia) akizindua Chuo cha Serikali za Mitaa Tawi la Shinyanga, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akikata utepe kuzindua Chuo Cha Serikali za Mitaa Tawi la Shinyanga
Muonekano wa Jengo la Chuo Cha Serikaliza Mitaa Tawi la Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru ambao ulikuwa ukienda kuzindua Chuo Cha Serikali za Mitaa Tawi la Shinyanga.

Mwenge wa Uhuru wazindua Chuo Cha Serikali za Mitaa Shinyanga

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBIO za Mwenge wa Uhuru Kitaifa umezindua Rasmi Tawi la Chuo Cha Serikali za Mitaa (Hombolo) katika Manispaa ya Shinyanga.

Chuo hicho kimezinduliwa leo Julai 28,2023, na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim.

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dk. Michael Msendekwa, amesema kitaanza masomo Rasmi Oktoba 16 mwaka huu kwa kudahili wanafunzi 800.

"Chuo hiki kitakuwa na Kozi Nne ya Utawala, Maendeleo ya Jamii, Uhasibu wa Fedha, na usimamizi wa Rasilimali watu,"amesema Dk. Msendekwa.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, amesema Chuo hicho kitakuza Sekta ya Elimu mkoani Shinyanga, kuchagiza uchumi na kuzalisha wataalamu ambao watalisaidia Taifa na kusongambele kimaendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amewataka wazazi wachangamkie fursa ya kusomesha watoto wao katika Chuo hicho kwa kupata elimu na kutimiza ndoto zao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464