NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI WILAYANI KISHAPU


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji akagua utekelezaji miradi ya maji wilayani Kishapu.

Na Marco Maduhu,KISHAPU

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameanza ziara mkoani Shinyanga ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji.

Ameanza ziara hiyo jana kwa kukutana na viongozi wa Mamlaka zote za Maji mkoani Shinyanga katika ukumbi wa Mikutano KASHWASA, pamoja na kutembelea baadhi ya Miradi ya Maji wilayani Kishapu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akiwa katika mradi wa maji Masanga- Ndoleleji.

Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi hiyo ya Maji wilayani Kishapu, amesema ameridhishwa na utekelezaji wake kwa kuzingatia thamani ya fedha pamoja na kujengwa kwa viwango.

"Wizara imeridhishwa na miradi ya maji wilayani Kishapu ambayo imetekelezwa na RUWASA,"amesema Mhandisi Luhemeja.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Ameagiza pia miradi ya maji ambayo bado inaendelea kutekelezwa wilayani humo kasi iongezeke na kukamilishwa kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.
Tangi la Mradi wa Maji Masanga-Ndoleleji wilayani Kishapu.

Katika hatua nyingine, ameziagiza Mamlaka zote za Maji mkoani humo, kutumia vyanzo vya uhakika vya maji hasa Maji kutoka Ziwa Victoria, ili miradi hiyo isikose maji na kuendelea kuhudumia wananchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, akipitia nyaraka za utekelezaji mradi wa maji.

"Sioni sababu ya vijiji vilivyopo Mikoa ya Kanda ya Ziwa kukosa huduma ya maji na wakati kuna Maji kutoka Ziwa Victoria, tumieni chanzo hiki kutoa huduma ya maji na kufikia asilimia 90," amesema Mhandisi Luhemeja.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa fedha na kutekelezwa miradi ya maji wilayani humo, kwamba awali hali ilikuwa mbaya lakini sasa hivi vijiji vichache vimesalia kupata maji.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela, amesema katika mwaka fedha (2023/2024) wanatarajia kupokea kiasi cha fedha Sh.bilioni 28.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kishapu Mhandisi Dicksoni Kamazima, amesema hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wilayani humo ni asilimia 56 na kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafikisha asilimia 90.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kishapu Mhandisi Dicksoni Kamazima.

Nao baadhi ya Wananchi wa wilaya ya Kishapu, wameipongeza Serikali kwa kuwatekelezea miradi ya maji, nakuomba ikamilishwe kwa wakati ili waanze kunufaika na huduma hiyo ya Majisafi na salama.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, wakwanza (kulia) akiendelea kukagua miradi ya Maji wilayani Kishapu.
Tangi la Mradi wa Maji Lagana- Igaga na Isagala.
Tangi la Mradi wa Maji Gundangali wilayani Kishapu.
Mfundi wakiendelea kuunganisha  Mabomba katika Mradi wa Maji. 
Chanzo cha Maji Mto Tungu.
Awali Mkurugenzi wa (KASHWASA) Mhandisi Patrick Nzamba, akiwasilisha taarifa uzalishaji wa Maji kutoka Chanzo cha Ziwa Vitoria Ihelele kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Viongozi wa Mamalaka za Maji mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao chao na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja,akiwa wilayani Kishapu katika Ofisi za Mkuu wa wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,alipofika kupata taarifa na kukagua miradi ya maji wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza katika ziara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akiangalia nyaraka yenye taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Maji wilayani Kishapu.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kulia)akiwa na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.
Viongozi wa Mamlaka za Maji wakiwa wilayani Kishapu katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
Kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji wilayani Kishapu kikiendelea.
Viongozi wa Mamlaka za Maji wakiwa wilayani Kishapu katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kuhitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji wilayani Kishapu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464