MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA KWA KISHINDO


MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA KWA KISHINDO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MWENGE wa Uhuru kitaifa umezindua, kutembelea, kufungua na kuweka mawe ya msingi katika Miradi 10 ya Maendeleo Manispaa ya Shinyanga.

Mwenge huo wa Uhuru katika Manispaa ya Shinyanga umekimbizwa umbali wa kilomita 72.5 na kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya Sekta ya Afya, Elimu, Mazingira, Miundombinu ya Barabara, Ujasiriamali, na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia pia mikopo ya asilimia 10.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo, amesema miradi yote ni mizuri na amepitia nyaraka zote na kujiridhisha kuwa imetekelezwa kwa ubora.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akikata utepe kuzindua mradi wa maendeleo wa vijana.

“Miradi yote tumeipitia iko vizuri ndiyo maana hakuna hata mradi mmoja ambao tumeukataa, na ile ambayo ina dosari ndogo ndogo ifanyieni maboresho zaidi,”amesema Kaim.

Aidha, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa wito kwa Wahandisi wa Halmashauri miradi hiyo waisimamie vizuri ili itekelezwe kwa ubora na kuonekana thamani ya fedha.
Mwenge wa Uhuru ukizindua Miradi ya Maendeleo.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo, amewataka wananchi wa Shinyanga kuendelea kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.

Naye Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi jimboni humo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akiwa wameushika Mwenge wa Uhuru.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu (2023) inasema' Tunza Mazingira,Okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa.
Usafi wa Mazingira.

Mwenge huo wa Uhuru kesho utakimbizwa katika wilaya ya Shinyanga.
Uzinduzi wa Vyumba 6 vya Madarasa,na Ofisi Mbili za Walimu katika Shule ya Msingi Bugweto.
Uzinduzi wa Mabasi Madogo Mawili mradi wa vijana kuwawezesha kiuchumi kupitia fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri asilimia 10.
Uzinduzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa, (Hombolo) Tawi la Shinyanga.
Jengo la Chuo Cha Serikali za Mitaa (Hombolo) Tawi la Shinyanga.
Uzinduzi Mradi wa Maji Bugayambelele.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, (kushoto) akiwa na Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi wakimtwisha Ndoo ya Maji Mwanamke Fotunata Malongo Mkazi wa Bugayambelele.
Jengo la wagonjwa wa Nje Kituo cha Afya Kambarage.
Ufunguzi wa Majengo kituo cha Afya Kambarage.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akiwa katika Kituo cha Afya Kambarage.
Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu akigawa Net kwa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage.
Mbunge wa Vitimaalu Mkoani Shinyanga Christina Mzava akigawa Net kwa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage.
Uzinduzi wa miradi ya maendeleo ukiendelea.
Mbunge wa Vitimaalumu Mkoani Shinyanga Christina Mzava akishiriki ujenzi wa miradi.
Viongozi wakishiki Shughuli za ujenzi wa miradi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Vitimaalu Mkoani Shinyanga Christina Mzava akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
iongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akiwa na wakimbiza Mwenge wa Uhuru.
Ukaguzi wa miradi ukiendelea kabla ya kuzinduliwa, kufunguliwa na kuweka Mawe ya Msingi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464