Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simon Belege (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze.
Mwenge wa uhuru wamulika miradi 9 ya maendeleo wilayani Shinyanga, Wananchi wahimizwa kupanda miti utunzaji Mazingira
Na Marco Maduhu,SHINYANGA.
Mbio za Mwenge wa uhuru umemulika Miradi 9 ya Maendeleo wilayani Shinyanga.
Mwenge huo umekimbizwa leo Julai 29,2023 wilayani Shinyanga umbali wa kilomita 94.2 na kukagua, kuona, kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi Miradi ya Maendeleo 9 wilayani Shinyanga, yenye thamani ya Sh.bilioni5.3
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Abdalla Shaib Kaim, akizungumza kwenye miradi hiyo, amesema mara baada ya kukagua nyaraka mbalimbali amejiridhisha kuwa iko sawa na kuagiza penye dosari ndogo ndogo pafanyiwe marekebisho.
"Mwenge wa uhuru umeridhika na Miradi ya Maendeleo wilayani Shinyanga," amesema Kaim.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akikata utepe kuzindua miradi ambayo imemulikwa na Mbizo wa Mwenye wa Uhuru.
Aidha, akizindua klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Kituli, ametoa wito kwa wananchi kupanda miti kwa wingi pamoja na kutunza mazingira hali ambayo pia itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akipanda Mti mara baada ya kumaliza kuzindua Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Kituli.
Naye Mbunge wa Solwa Ahmed Salum, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi wilayani humo na kutekelezwa miradi mingi ya maendeleo.
Mbunge wa Solwa Ahmes Salum akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Miradi ya maendeleo ambayo imemulikwa na Mwenge wa Uhuru wilayani Shinyanga ni Mradi wa Maji wa Ishinabulandi, kikundi cha vijana wabunifu, uzinduzi wa gari la wagonjwa, Klabu ya wapinga Rushwa na Mazingira Shule ya Sekondari Kituli na vyumba vinne vya madarasa.
Pia Mwenge huo umezindua Kiwanda kidogo cha Nafaka na kuongeza thamani ya zao la Mpunga na Ndege wa Mapambo.
Miongoni mwa viongozi wakimbiza Mwenge Kitaifa akiangalia ubora wa Mchele katika Kiwanda cha Nafaka Didia.
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu 2023 inasema Tunza Mazingira,Okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe Hai kwa uchumi wa Taifa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru tayari kwa kumulika Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru tayari kwa kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani humo.
Mkugugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simon Belege akiwa ameushuki Mwenge wa Uhuru tayari kwa kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani humo.
Mbunge wa Vitimaalu Mkoani Shinyanga Christina Mzava akiwa ameushuki Mwenge wa Uhuru tayari kwa kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akiwa ameushuki Mwenge wa Uhuru tayari kwa kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani humo.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge huo wa Uhuru kwa ajili ya kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani Shinyanga.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge huo wa Uhuru kwa ajili ya kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani Shinyanga.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge huo wa Uhuru kwa ajili ya kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani Shinyanga.
Viongozi wakiendelea kuushika Mwenge huo wa Uhuru kwa ajili ya kumulika Miradi ya Maendeleo wilayani Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akiweka jiwe la Msingi Mradi wa Maji wa Masengwa awamu ya Pili ambao umetekelezwa na RUWASA.
Tangi la Mradi wa Maji Masengwa awamu ya Pili.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, akimtwisha Ndoo Mwanamke Kichwani Mkazi wa Kijiji cha Ishinabulandi na kumtua Ndoo hiyo kama ishara kwamba miradi ya maji inatekelezwa kwa ajili ya kumtua Ndoo kichwani Mwanamke
Mwenge wa Uhuru ukipita kuona mradi wa vijana wabunifu Kata ya Usanda ambao wamebuni pia na utengenezaji wa Gari.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akikata Utepe kuzindua gari la Wagonjwa ambalo limetolewa na Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5.
Muonekano wa gari la wagonjwa ambalo limetolewa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, akizundua Klabu ya wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Kituli
Klabu ya wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Kituli.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, akipanda Mti kuzindua Klabu ya Mazingira katika Shule ya Sekondari Kituli.
Mbunge wa Solwa Ahmed Salum akipanda Mti wakati wa uzinduzi wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Kituli.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simoni Belege akipanda Mti wakati wa uzinduzi wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Kituli.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simoni Belege akipanda Mti wakati wa uzinduzi wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Kituli.
Upandaji Miti ukiendelea.
Upandaji Miti ukiendelea.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akizundua vyumba 4 vya Madarasa Shule ya Sekondari Kituli.
Muonekano wa vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Kituli.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akikagua uimara wa viti na meza katika vyumba vipya ya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kituli.
Kiwanda cha kuchakata Nafaka na kuongeza thamani ya zao la Mpunga Didia, akikizinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akifunga Rasmi Kiwanda hicho cha Kuchakata Nafaka na kuongeza Thamani ya zao la Mpunga kilichopo Didia
Muonekano wa kiwanda hicho kwa ndani.
Mmoja wa viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akiangalia ubora wa Mchele.
Ndege wa Mapambo ambao pia walionwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Ndege wa Mapambo.
Picha ya pamoja ikipigwa katika Kiwanda cha kuchakata Nafaka na kuongeza thamani ya Zao la Mpunga Didia
Awali Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akiendelea na umulikaji wa miradi ya maendeleo wilayani Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464