Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude aweka Msukumo wa kukamilisha Ujenzi wa Miradi ya Boost ikamilike Julai 15,2022
Mhe. Mkude ameyabainisha hayo jana alipofanya Ziara ya kikazi ya Kutembelea Miradi hiyo ambayo inathamani ya Shilingi Bilioni 1.5
Mhe. Mkude ameridhishwa na kazi zinazoendelea kufanyika katika sehemu mbalimbali zinazotekeleza Miradi hiyo ya Boost na kutoa Muda kwa Mafundi kufikia tarehe 15 Julai wawe wamekamilisha ujenzi huo.
"Nimeridhishwanna utendaji kazi wa miradi sehemu nyingi wapo hatua ya ukamilishaji ambayo ni sawa na asilimia 80. Hivyo basi wito wangu ni kuona kila fundi kufikia Tarehe 15 Julai awe amekamilisha mradi wake." Amesema Mkude
Aidha Mhe. Mkude amewataka Wananchi kuwa wazalendo na kuitunza miradi mbalimbali ambayo inaendelea kutekelezwa Chini ya Serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464