DC MKUDE AZINDUA TAMASHA SANJO YA BUSIYA WILAYANI KISHAPU


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude amezindua rasmi Tamasha la Sanjo ya Busiya ambalo huadhimishwa kila Mwaka Tarehe 7 Julai.

Tamasha hilo limezinduliwa jana.

Sanjo ya Busiya huadhimishwa kila Mwaka Tarehe 07 Julai katika kata ya Ukenyenye Tarafa ya Negezi ikiwa na lengo la kuwaunganisha Pamoja wanaKishapu katika huduma mbalimbali za Kijamii.

Katika uzinduzi huu Mhe. Mkude ametumia furusa hiyo kuwapongeza sana Jamii ya ya Kisukuma Hasa utemi wa Busiya kwa kitu kizuri wanavyokifanya cha kuenzi utamaduni na kukuza sanaa kupitia Maadhimisho hayo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.

"Ninawashukuru sana Ndugu zangu Wasukuma kwanza ni wakarimu na Wacheshi ninaomba niwapongeze sana kwa hihi kitendo cha kuwa wamoja na kujijengea tabia ya kuadhimisha siku ya Saba Saba kw kuenzi Tamaduni kati maadhimisho haya mnakuza Sanaa katika jamii hii katika utamaduni, Kwa hiyo kupitia Utamaduni na Michezo tunaweza kufanya mambo mbalimbali ya kukuza Sanaa Nchini. Nimppngeze sa Mtemi Makwaaiya kwa kuona inapendeza kuadhimisha Siku ya SabaSaba kwa kuenzi Utamaduni na Watu wa Busiya.

Kwa Upande wake Mtemi wa Busiya Ndugu. Edward Makwaya Amemshukuru sana Mhe. Mkude kwa kuitikia wito wa kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,
Mtemi wa Busiya Edward Makwaya.

"Mhe. Mkude nakushukuru sana kwa kuitikia wito huu kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hata ya Sabasaba hii inaonyesha jinsi gani unavyoshirikiana na jamii katika kila nyanja.

Aidha Mhe. Mkude alipata Wasaa wa kuelezea mazuri yanayofanyika katika kipindi cha Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan ikiwemo miundo mbinu ya Maji, Barabara, Umeme na Miradi ya Afya pamoja na Elimu inavyozidi kutekelezwa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464